MBIO
za Mwenge wa Uhuru Katika mkoa wa Manyara utakimbizwa katika
Halmashauri tano za mkoa huo na kutembelea miradi 39 ya maendeleo yenye
thamani ya shilingi Bilioni 23.2.
Miradi
17 yenye thamani ya shilingi Bilioni 20.7 itawekwa mawe ya msingi,
Bilioni 1.6 itafunguliwa huku mingine Tisa yenye thamani ya shilingi
milioni 843.7 ikitembelewa.
Aidha
katika mkoa wa Manyara Mwenge utakimbizwa Katika Mamlaka za Serikali za
mitaa Saba ambazo ni Simanjiro,Kiteto,Babati mji,Babati
wilaya,Hanang,Mbulu wilaya na Mbulu mji kwa mzunguko wa kilometa.
Mkuu
wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere ameahidi kusimamia vyema
Mwenge huo Kipindi chote utakapokuwa ndani ya Manyara.
Mwenge
wa Uhuru mwaka 2022 leo Juni 13 umeanza kukimbizwa Katika mkoa wa
Manyara ukitokea mkoa wa Kilimanjaro na kilele chake ni Juni 19.
Akikabidhi
Mwenge huo kwa mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere, mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai amesema katika mkoa wake Kiongozi
wa Mbio za Mwenge kitaifa Sahil Geraruma amekagua na kufungua miradi 38
yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 13.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...