Na John Walter-Babati


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Sahil Geraruma amewataka viongozi na watendaji wanaosimamia ujenzi wa miradi ya Maendeleo katika maeneo yao, waongeze kasi ikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa ili kuwapa fursa wananchi kunufaika na miradi hiyo.


Geraruma ametoa wito huo leo Juni 15,2022 wakati akizungumza na mamia wa wakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoani Manyara mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la kituo cha afya cha Madunga kinachojengwa katika kijiji cha Gidng'war kwa fedha za serikali kuu zilizotokana na tozo ambapo Halmashauri hiyo ilipokea mgao wa shilingi Milioni 250,000,000.00 kwa ajili ya mradi huo.


"Nitumie fursa hii kuwaomba viongozi na watendaji wanaosimamia mradi huu waendelee kushirikiana na kufanya kazi kwa kasi zaidi ili kukamilisha ujenzi huu kwa wakati uliopangwa ili kuwapa fursa wananchi".


Amesema lengo la Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kujenga vituo vingi zaidi ili wananchi wasitembee umbali mrefu kutafuta huduma za afya.


Kiongozi wa mbio za Mwenge Sahil Geraruma, kabla ya kuweka jiwe la msingi alikagua majengo ya kituo hicho ambapo amesema ameridhishwa na ujenzi wake na hasa kiwango cha ubora kilichopo.


Akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hicho afisa mtendaji wa kata ya Madunga Halima Chambali, alisema kuwa lengo la mradi huo ni kutoa huduma bora za matibabu kwa wakazi wa Madunga pamoja na vijiji jirani ambapo huduma zitakazopatikana ni uchunguzi wa afya,huduma ya upasuaji,matibabu ya magojwa mbalimbali,elimu ya afya pamoja na ushauri wa afya na mazingira.Gharama za ujenzi wa mradi kwa awamu ya kwanza ni shilingi milioni 284,105,000 na nguvu za wananchi ni shilingi milioni 34,105,000 na kazi imefikia hatua ya ukamilishaji wa majengo mawili ya awamu ya kwanza na kichomeo taka na fedha zilizolipwa ni shilingi 137,472,587.04.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma mbalimbali hususani za afya pia kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya.


Mradi huo uliopo kwenye eneo la ukubwa wa hekari 8.5 unaohusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD),jengo la maabara na kichomea taka na kutekelezwa kwa njia ya FORCE ACCOUNT linatarajiwa kukamilika juni 30 mwaka huu kwa awamu ya kwanza.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...