Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amewataka wanawake wa mkoa huo kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kazi zote anazofanya kwa kuwa kwa sasa nchi imetulia.

Bi,Kevela amesema nchi imekuwa na amani na utulivu mkubwa kwa kuwa kuna wakati watu makundi mbali mbali wakiwemo wafanyabiashara walikuwa wakiishi kwa kuhofia juu ya biashara zao.

“Ninachofurahia ni amani,nchi imetulia yaani unaamka unajua unaenda shambani bila bughudha yeyote,lakini kuna kipindi mfanyabiashara unalala unawaza sijui kesho nitakutana na magereza au nini.Lakini sasa hivi amani nchi imetulia”alisema Scolastika Kevela

Vile vile amebainisha kuwa Rais Samia ameendelea kufanya vizuri na kuboresha mahusiano ya ndani na kimataifa kwa kuwa nchi ya Tanzania sio kisiwa na kupelekea Mtanzania kwenda nchi yeyote.Amebainisha haya wakati akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo wilaya ya Njombe alipofanya ziara katika jimbo la Lupembe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...