Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo tarehe 06/06/2022 imefanya mazungumzo na Shirika la Siloam Center for the Blind la nchini Korea. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za TET zilizopo Jijini Dar es salaam.
Mazungumzo
hayo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo kati ya TET na shirika hili
wenye lengo la kushirikiana katika kuandaa vitabu vya Breli kwa ajili
ya wanafunzi wasiona wa ngazi zote za elimu nchini.
Katika
Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Siloam Center for the Blind
Ndugu Dong ic Choi ameahidi kuwa kwa mwaka huu wa fedha shirika
litachapa vitabu katika maandishi ya Breli kwa vitabu vyote vya Kiada
vya Ngazi ya Elimu ya Sekondari vitakavyoandaliwa na TET.
Katika
ushirikiano huu Siloam watazalisha vitabu Nchini Korea kwa kutumia
technolojia ya kisasa na kuvisafirisha mpaka Tanzania, ambapo TET
itafanya jukumu la kuvitoa Bandarini na kuvisambaza katika shule husika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ameshukuru na
kuahidi kutimiza majukumu yao kwa wakati ili kuhakikisha kuwa wanafunzi
wasioona wanapata haki yao ya msingi ya kupata vitabu vya kujifunzia kwa
wakati. Vitabu hivi hugawiwa kwa uwiano wa vitabu vitatu kwa
mwanafunzi mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...