Na.Khadija Seif , Michuzi TV
MICHUANO ya Ndondocup yafungua njia Kwa zaidi ya Miaka 9 Kwa vijana wa mtaani, yarudi tena Kwa kishindo kupitia tv3 ndani ya king'amuzi cha Startimes.
Tv3 imepata kibali cha kudhamini michuano hiyo na kuonyesha mubashara kuanzia julai 3 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Tv3 Ramadhan Msemo, amesema kuwa Tv3 wameona sehemu sahihi na kupata haki na nafasi ya kutoa nafasi kuonekana kuanzia ufunguzi hadi Fainali.
"Ndondo cup ni sehemu ya kuwalea watu kimichezo na kuona vipaji tofauti vya vijana ambao walikuwa mtaani, walikuwa hawajui watapata lini nafasi ya kucheza na kuonekana hivyo kupitia ndondocup inawapa nafasi vijana.
Aidha,Msemo ameongeza kuwa ndondocup ni daraja ambalo linagusa
Kila sekta ikiwemo sekta ya Afya, michezo pamoja na biashara Kwa ujumla.
Aliongeza kuwa Katika mashindano hayo imeshangaza kuona timu ya Mshikamano city ina kocha mwanamke ni Jambo kubwa Sana na lenye kuleta usawa wa kijinsia na kuwapa vipaumbele jinsi ya kike na yote yametokana na michuano hii ya Ndondo Cup.
Nae Mratbu wa michuano hiyo Yahya Mohamed, amesema udhamini huo utaenda kuleta Mabadiliko makubwa na matayarisho Kwa vijana kujiandaa na michuano mikubwa zaidi na Kwa Sasa michuano ya ndondocup Imefikisha miaka 9 tangu ianzishwe na imekua miaka yenye Mapinduzi makubwa zaidi.
Mohamed ameongeza kuwa mfumo wa uendeshaji wa michuano hiyo unafata taratibu za Mfumo wa uendeshaji wa kombe la Dunia Kwa kusajili Timu 32 na Kwa mara ya kwanza Mechi y ufunguzi ilifanyika shule ya makurumla Jijini Dar es salaam lakini Kwa mwaka huu imekua tofauti kutokana na timu takribani 72 kutaka kushiriki michuano hiyo.
Pia ametaja mafanikio tangu kuanza Kwa michuano hiyo ya ndondocup ikiwemo kuwapa nafasi vijana kuonekana na kuzalishwa Kwa vipaji vingi vipya na vizuri mfano halisi kelvin sabato maarufu kama "Kiduku, idi Suleiman Nado .
"Kuwasaidia wachezaji kupata nafasi na kadri muda ulivokua ukisonga makocha walikua wakihitaji Mabadiliko hivyo hata makocha na waamuzi wao ni wasomi na Wana vyeti vilivyokidhi kanuni za kuchezesha michuano hiyo.
.Timu jaribu zote zinazoshirki ndondo cup wasomi na Wana vyeti na kutambulika .
"Kuna waamuzi kama Ramadhan Kayoko,Heri Sasi ni Misingi bora ya michuano ya ndondocup tumekuwa daraja la kusaidia, walikuwa hawana nafasi, wakapata nafasi wameitumia vizuri ".
Hata hivyo zawadi Kwa Mshindi wa michuano hiyo milioni 20 Huku Mshindi wa pili milioni 10 na milioni 1 kwenda Kwa kikundi bora cha ushereheshaji uwanjani.
picha ya pamoja kati ya wadhamini wa michuano ya ndondocup Mkurugenzi wa tv3 Ramadhan Msemo, Mratibu wa michuano hiyo yahya Mohamed,Meneja Masoko wa Kampuni ya startimes David Malissa ,Balozi wa Ndondocup mbwiga mbwiguke na mdhamini mwenza kutoka clouds issa Masoud wakati wa kutambulisha rasmi kuwa tv3 imepata kibali cha kuonyesha mubashara michuano hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...