Na Vero Ignatus,Arusha.


Wakati Serikali ikiendelea na juhudi za kuhakikisha vijana wanajiajiri wenyewe , baadhi ya vijana Mkoani Arusha wamekuja na ubunifu wa kuchakata baadhi ya taka za plastiki na kugeuza kuwa bidhaa mbadala za mbao ili kulinda na kutunza mazingira

"Tumeamua kutumia taka hizi kuwa mbao kwa ajili ya kutengeneza samani mbalimbali kwa matumizi ya kijamii kwa mfano Nguzo, meza, viti, vigae vya sakafuni, zikiwa na nakshi mbalbali" Alisema Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Green Venture LMD Ndg Edgar Tarimo"

Vijana hao ambao waliweza kubadilisha taka hizo ambazo zinatupwa holela, na kuchafua mazingira kuwa mbao kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali Kama viti, meza, madawati, na nguzo walisema kuwa, fursa hiyo ilitokana Mara baada ya kuona mifuko ya plastik inachukua muda mrefu kuoza

Akitoa taarifa ya kiwanda hicho mbele ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kaskazini NEMC ,Mkurugenzi wa kiwanda hicho GREEN VENTURE LTD Edgar Endmund amesema wazo hilo alilipata mara baada ya utafiti mdogo alioufanya na kugundua kuwa taka za plastiki zinachukua muda mrefu kuoza ,hivyo akachuka kama fursa ya kujipatia kipato.

"Kupitia kiwanda hiki tumeweza kutoa fursa mbalimbali kwa vijana zaidi ya 100 wa nje na tuna mkakati wa kuawaajiri vijana wengine wa ndani ili kuweza kupeana zamu ya kufanya uchakataji mkubwa kwani kiwanda kinaendekea kukua.

Kwa upande wake Mhandisi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kaskazini Nancy Nyenga alisema kuwa katika kuendeleza wiki ya mazingira wameweza kuona ubunifu mbalimbali na kugundua plastiki zilizo zoeleka zinaweza kugeuzwa na kuwa Samani za kuvutia

"Tumefurahishwa na kazi ya vijana Hawa kwani nawaomba wanajamii wanaozalisha hizo taka kuzikusanya na kuzirejesha kwenye viwanda hivyo ili kuweza kuwarahisushia wakati wa uchakataji wa taka hizo kwa kutunza mazingira"Alisema Nancy

Hata hivyo aliwataka kutafuta sehemu mzuri ambayo atafanya kazi kwa uhuru na kuepukana na madhara yanayotokana na Moshi unaotokana na uzalishaji huo huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa vijana hao ili kuweza kufikia Malengo yao na hatimaye kujikwamua kiuchumi

Kwa upande wake Afisa mazingira kutoka Halmashauri ya (W)ya Meru Charles Makama Mboya amewaoongeza vijana hao kwa ubunifu walioufanya, huku akiwashauri kuboresha teknolojia yao ili waweze kuzalisha bidhaa ambazo zinazoendana na mazingira huku aliwataka pia kuweka mazingira rafiki ya Kiafya kwa watu wanaowazunguka.

Naye Afisa mazingira Halmashauri ya (W) Meru Naima Temba amesema wametembelea viwanda vidogo vinavyochakata taka ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni yao isemayo taka pesa taka ni Ajira,ikiwa imelenga kuhamasisha vijana kujikita kuchakata taka kuwa Mali nyingine na kuwa bidhaa nyingine zinazoweza kutumika na kuzalisha Ajira za watu mbalimbali.

Hivi karibuni Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo Duniani (UNDP)linashirikiana na Chuo Kikuu cha Taifa, SUZA visiwani Zanzibar kutekeleza mradi wa kuibuka na mbinu bora zaidi za kukusanya taka ngumu ili kufanikisha lengo namba 12 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs

Kwa mujibu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP26) huko Glasgow nchini Scotland, kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi tarehe 12 Novemba 2021 ulifanikiwa ,ambapo Umoja wa Mataifa katika harakati za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi,Lengo likiwa ni kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa na hivyo kupunguza kiwango cha joto duniani.

Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC ambao unajumuisha michango na ahadi zilizowekwa kitaifa na nchi mbalimbali kama hatua madhubuti za kupunguza athari za ongezeko la kiwango cha joto duniani unapaswa kutekelezwa kama ilivyokubaliwa.

Aidha changamoto ya kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa asilimia 45% ifikapo mwaka 2030 ni muhimu hivyo Umoja wa Mataifa unabainisha kwamba, kuna haja ya kutekeleza kwa vitendo upunguzaji wa nyuzi joto 1.5C kama ilivyobainishwa kwenye Makubaliano ya Paris chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi.

Kila nchi itaamua kiwango cha mchango wake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,Kiwango hicho kitategemea uchumi wa nchi husika na pia kiasi cha uzalishaji wa gesijoto, huku Kuongeza uwekezaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa angalau asilimia 50% ya fedha za jumla za ufadhili wa umma wa mabadiliko ya tabianchi.
Taka ambazo huchakatwa na kugeuzwa bidhaa kwaajili ya matumizi mengine ikiwemo mbao,nguzo,madawati,meza viti na marumaru 
Mhandisi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kaskazini Nancy Nyenga
Mkurugenzi wa kiwanda hicho  GREEN VENTURE LTD Edgar Edmund  akielezea namna ambavyo wanachakata taka na kuzigeuza bidhaa mbalimbali kwaajili ya matumizi mwengine
Kwa upande wake Afisa mazingira kutoka Halmashauri ya (W)ya Meru Charles Makama Mboya 
Taka zikiwa zimechakatwa tayari kwaajili ya kubadilisha kuwa bidhaa kwajaili ya matumizi mengine
Halmashauri ya (W) Meru Naima Temba akielezea namna ambavyo Kampeni yao isemayo taka pesa taka ni Ajira,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...