Na Mwamvua Mwinyi,Mafia
Nyumba takriban 1,000 ambazo zimeezekwa kwa makuti, katika kisiwa cha Mafia ,zinatarajia kuboreshwa kwa kuezekwa kwa mabati ili kujiepusha na majanga ya Moto .
Mpango huo unafuata baada ya Taasisi ya Khidma tul Ummah, kujenga nyumba saba ,kwa ajili ya wahanga wa janga la moto ambao mnamo mwezi Septemba mwaka 2021 nyumba zao ziliteketea kwa moto.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Khidma tul Ummah, Sheikh Arif Surya alibainisha mpango huo wakati akikabidhi nyumba hizo saba zilizojengwa na taasisi hiyo.
"Wanufaika wa nyumba hizo saba hapo awali walikuwa wakimiliki nyumba za udongo na nyasi lakini kwa kupitia msaada huu ,wameweza kuingia katika nyumba za kisasa zilizojengwa kwa tofali na bati kwa gharama ya sh.milioni 72.3 ."amesema.
Wakati akimshukuru Sheikh Arif na Taasisi ya Khidma tul Ummah, Mkuu wa Wilaya ya Mafia ya Mafia, Mhandisi Martin Ntemo aliwapongeza wafadhili hao kwa mchango huo mkubwa kwa wanajamii wa Mafia .
Aliwataka wanufaika kuhakikisha kuwa nyumba hizo zinatunzwa na kwamba zinakuwa chachu kwa wananchi wengine kujenga nyumba zinazofanana na hizo ili kuboresha mazingira na muonekano wa kisiwa hicho ambacho bado zipo nyumba nyingi za makuti ambazo ni hatari kwa moto hasa katika vipindi vyaa kiangazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...