Na Mwandishi Wetu, Michuzi Tv
Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS imeandaa mafunzo kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii Tanzania (JUMIKITA) lengo likiwa ni kuwajengea uwelewa wanahabari hao kuhusu maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.
Mafunzo hayo yameanza leo Juni 14, 2022 Mkoani Iringa na yatahitimishwa hapo kesho Juni 15. kwa kushirikisha Waandishi wa habari na Wahariri wa Mitandao ya Kijamii nchi nzima.
akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo Mwanasheria Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mary Senapee amesema kuwa ni Kinyume cha Sheria za Takwimu kufanya yafuatayo; Kutoa taarifa/takwimu za uongo, Kumshawishi mtu asishiriki zoezi la Takwimu,Kujifanya Afisa wa Takwimu na Kutumia Takwimu za Sensa kwa taarifa zako binafsi
aidha alitaja kuwa n i kosa kisheria kumzuia Afisa wa Takwimu kutekeleza majukumu yake ya ukusanyaji wa Takwimu pia ni kosa kisheria kukataa au kuacha kwa makusudi kujaza fomu au nyaraka zozote za ukusanyaji takwimu.
Sensa ya kwanza ya mwaka 1967 ilipata ya watu milioni 12.3, sensa ya pili ya mwaka 1978 ilipata watu milioni 17.5, sensa ya tatu ya mwaka 1988 ilipata nidadi ya watu milioni 23.1, sensa ya nne ya mwaka 2002 ilipata watu milioni 34.4, sensa ya tano ya mwaka 2012 ilipata idadi ya watu milioni 44.9 na sensa ya sita ya mwaka 2022 inakadiriwa kupata watu milioni 61.3
Waandishi wa habari kutoka Mitandao Mbali mblai ya kijamii Wakiwa katika Mafunzo Maalum ya Umuhimu wa Sensa ya watu na Makazi, Mafunzo hayo amabyo yameratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Kwa kushirikiana na Jumuiya Mitandaoni ya kijamii Tanzania (JUMIKITA)
Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Said Amir akitoa Mafunzo Kwa Waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii mkoani Iringa kuhusu maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.Mwanasheria Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mary Senapee akitoa Mafunzo Kwa Waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii Tanzania (JUMIKITA) mkoani Iringa kuhusu maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...