NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
KAIMU
KATIBU TAWALA Mkoa wa Morogoro, Bw. Herman Tesha amewaasa Maafisa Utumishi na
Utawala nchini kuwasaidia wafanyakazi katika mchakato wa kutaarifu ili kupata
stahiki zao kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) pindi wanapopatwa na
changamoto za kuumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.
Ameyasema
hayo wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa hao kuhusu Huduma za Fidia na masuala ya Usalama na Afya Mahali pa kazi mkoani Morogoro, hivi
karibuni.
“Najua mtakuwa mmejifunza mambo mengi mapya ambayo hamkuwa nayo hapo awali, mimi binafsi nimeshawahi kuhudhuria mafunzo kama haya na nimefaidika sana. Nitoe rai kwenu nyote mtumie elimu mliyoipata kuwasaidia wafanyakazi wenu kupata stahiki zao pindi wanapoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi na kwa kufanya hivyo mtakuwa pia mmeusaidia Mfuko kutimiza lengo la kuanzishwa kwake.” Alisisitiza na kutoa mfano… "Mimi mwenyewe ofisini kwangu, watumishi wetu watatu wamefaidika na Mfuko huu tena bahati mbaya zaidi mmoja alifariki lakini ukweli wategemezi wake wanaendelea kufaidika na WCF.”
Kwa
upande wao washiriki wamefurahishwa na elimu waliyoipata na wameahidi kwa kupitia mafunzo hayo kila mmoja ataenda kutenda kwa usahihi kwa mujibu wa sheria na
miongozo.
“Huduma
ya Mtandao ninafahamu ni kitu kizuri sana kwa sisi waajiri kwani tunaweza
kuingia kwenye mtandao na kutoa taarifa kwa wakati na mtumishi ataweza kupata
stahiki yake kwa wakati.” Alisema Bi. Leila Komba, Afisa Utumishi Mwandamizi
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
“Sisi
tuliobahatika kupata mafunzo haya basi tukawafundishe wenzetu wakiwemo waajiri
wetu.” Alisema mshiriki mwingine Bi. Leticia Machibya kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali.
Aidha
Wameushukuru Mfuko kwa kutoa mafunzo hayo na wangependa yawe endelevu
Awali
akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Mkurugenzi wa
Huduma za Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulssalaam Omar, alisema hilo ni kundi
la kwanza la Maafisa Utumishi na Utawala au Maafisa Rasilimali Watu kutoka
katika taasisi za Umma kupata mafunzo hayo.
“Tumeanza kutoa elimu kama hii kwa Maafisa Utumishi kutoka katika Halmashauri”. Alifafanua Dkt. Omar.
“Tunafahamu
kuwa Maafisa Utumishi na Utawala ni kiungo muhimu sana katika kazi zetu kama
Mfuko wa Fidia, kwa sababu wafanyakazi wanapopata changamoto hatua ya kwanza
wanawataarifu ninyi na nyie mnao wajibu wa kumtaarifu Mkurugenzi Mkuu WCF kwa
niaba ya waajiri wenu, hivyo tumeona ni muhimu kwenu kupata elimu zaidi.”
Alisisitiza.
Mafunzo
hayo yalihusu uelewa wa jumla kuhusu WCF, Mafao ya Fidia yanayotolewa na Mfuko
na Jinsi ya kutoa taarifa za matukio endapo mfanyakazi ataumia, kuugua au
kufariki kutokana na kazi kwa njia ya mtandao.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF Dkt. Abdulsalaam Omar, akitoa Mada kuhusu Mafao yanayotolewa na Mfuko
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bw. Herman Tesha, akizungumza na Maafisa Utumishi na Utawala
Baadhi ya Maafisa Utumishi na Maafia Utawala kutoka taasisi za Umma, wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Bi. Tumaini Kyando kutoka WCF, akifuatilia majadiliano ya vikundi
Afisa Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi WCF, Bw. Robert Duguza, akifuatilia mijadala kwenye makundi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza na washiriki
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani Morogoro, Bw. Athumani Khalfan, akitoa mada kuhusu Sheria ya Fidia.
Meneja Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi, Bi. Naanjela Msangi, akitoa mada kuhusu usalama na afya mahali pa kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...