




Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Ndugu Reverien Ndukiriyo wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja wa kisasa wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex uliopo mkoani Makamba, Burundi.

Pichani baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kutoka wilaya ya Buhigwe, Kigoma wakiwa wamejumuika na wenyeji wa Burundi kama Ishara ya Ujirani mwema wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja mpya wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex uliopo Makamba nchini Burundi.

Chifu Mtwale Isambe Rugali Buliho wa himaya ya Heru Juu Buha kasulu Kigoma akionyesha uzalendo kwa majirani zake wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex, Makamba nchini Burundi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...