NA MWANDISHI WETU, SABASABA
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewaalika wanachama wake na wananchi kwa ujumla kutembeela banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyoanza Juni 28, 2022 kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Afisa Uhusuano Mwandamizi wa PSSSF, Bi. Fatma Elhady amesema imekuwa ni fursa nzuri kwa Mfuko kushiriki katika Maonesho hayo ili kuwawezesha Wanachama na wananchi kwa ujumla kupata taarifa za huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.
“Tunawakaribisha sana Wanachama wetu na wananchi kutembelea Banda namba 13 la Ushirikiano lililoko mtaa wa Mabalozi.” Alisema.
Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni "Tanzania Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji."
Wafanyakazi wa PSSSF na NSSF, wakiwa eneo la mapokezi kuwahudumia Wanachama na wananchi wanaotembelea Banda hilo la Ushirikiano.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...