Na Said Mwishehe, Michuzi TV

NOAMBA nikiri Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kusimama katika misingi ya yaki, haiko tayari kuona haki ya mtu inapotea.

Ndio Rais Samia tangu ameingia madarakani Watanzania tumeshuhudia haki ikipewa nafasi kubwa katika kila maamuzi yanayotolewa.Hakika Serikali ya Rais Samia imejipambanua kwenye kusimamia haki,haki,haki

Katika kutenda huko haki kuna mifano mingi inayoweza kutumika kama ushahidi, ndio kuna mifano mingi inayothibitisha hilo.Unaweza kuuliza ni ushahidi upi unaweza kutumika katika kuthibitisha hilo.

Ni hivi moja ya mfano ni pale ambapo Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu anapojitokeza na kueleza kuwa Serikali ya Rais Samia imemlipa kiinua mgongo chake alichokuwa anadai kwa muda mrefu baada ya kutumikia nafasi ya ubunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa kukumbusha tu Lissu alivuliwa ubunge Juni 28 mwaka 2018 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kutojaza taarifa za mali na madeni na kutoa taarifa kwa Spika wa Bunge mahali aliko.Wakati anavuliwa ubunge, mwanasiasa huyo alikuwa Ubelgiji akiendelea na matibabu baada ya kupigwa risasi 16 na watu wasiojulikana akiwa katika makazi yake Dodoma Septemba 2017.

Sote tunafahamu Lissu ametumia mbinu na njia mbalimbali kuomba alipwe mafao yake,lakini hakuna aliyemsikiliza, fedha aliyokuwa anadai ni pamoja na fedha ya matibabu yake.

Nakumbuka sarakasi za Lissu kudai mafao yake zilikuwa ni kwenye Serikali ya Awamu ya Tano.Nimeitaja kwa sababu ndio wakati aliokuwa akidai.Narudia tena hakupata nafasi ya kusikilizwa.Hakupata nafasi ya kusikilizwa ndani ya Bunge ambalo lilikuwa likiongozwa na aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai.Pamoja na kuumwa kwa muda mrefu Lissu alihakikisha anaipigania haki.

Awamu ya Sita chini ya Rais Samia kwa kuwa inaamini katika haki na haki ya mtu haipotei ikaona isiwe tabu.Rais Samia Februari mwaka huu akakutana na Lissu aliyekuwa nchini Ubelgiji.Lissu alifikisha kilio hicho baadaye alieleza kuwa ameahidiwa kusaidiwa.

Rais Samia ni mtenda haki, alimsikiliza Lissu yale yooote aliyoona anapaswa kumwambia ili amsaidie.Pia alimuomba Rais Samia kumsaidia kupata hati ya kusafiria, jambo ambalo alisema lilitekelezwa ndani ya muda mfupi.

Unajua nini ambacho kimetokea baada ya mazungumzo yale? Lissu ameamua kuvunja ukimya na kuelezea kwamba miezi miwili iliyopita alipigiwa simu na maofisa wa Wizara ya Fedha kumueleza fedha alizokuwa akidai amelipwa.Yaani chini ya Serikali Rais Samia Lissu mfukoni hayuko vibaya, mfuko umetuna mihela.

Ukweli uliopo kwa mazingira ya namna hiyo huna sababu ya kukaa kimya na kushindwa kutoa shukrani kwa Rais Samia, Lissu anakiri kuwa hana tatizo na Rais Samia kwani uongozi umejaa matumaini.Anaona kabisa kuna tofauti kubwa kati ya Awamu ya Sita na Awamu iliyopita.

Kwa aina hii ya staili ya uongozi ambayo Rais Samia ameamua kuitumia katika kuongoza nchi yetu ya Tanzania mbali ya kuleta faraja kwa Lissu imegusa pia watu ambao nao kwa namna moja au nyingine waliona kutotendewa haki .Ndio ukweli.

Nakumbuka miongoni mwa hotuba za mwanzo kabisa kuwahi kutolewa na Rais Samia ni Ile aliyokuwa akizungumza na Watanzania na kuwaambia huu ni wakati wa kushikamana na kubwa zaidi ni wakati wa kufutana machozi.

Kauli ya Rais Samia naiona imetumia kwa vitendo.Wengi waliokuwa wakitokwa machozi kwa kuamini wamekosa haki leo hii ni kicheko tu.Wanafuraha tele moyoni kwasababu Rais Samia ameamua kuwaondolea maumivu kwa kuhakikisha wanapata haki zao zinazostahili.

Watanzania wenzangu huu ndio wakati wa kumuunga mkono uongozi wa Rais Samia , no uongozi ambao hauna makuu, hauna make, ni uongozi ambao hauna Kash kashi.Ni uongozi ambao unatoa nafasi kwa kila mwananchi kufurahia nchi yetu .

Binafsi nafurahishwa na hatua ambazo Rais anachukua katika kuhakikisha hakuna mtu kuonewa,hakuna mtu kudhulumiwa .Ili Tanzania yetu iendelee kusonga mbele unahitaji Umoja na mshikamano na huwezi kuwa na umoja katikati ya kundi la watu wanaoishi na vinyonyo moyoni .Tundu Lissu anakuwa miongoni mwa Watanzania wanaosema hadharani Rais Samia ni mtenda haki.Na huo ndio uhalisia, Awamu hii inasimamia haki.

Hata hivyo kabla ya kuhitimisha ,nitumie nafasi hii kumueleza Lissu chini ya Rais Samia Watanzania wako salama kuliko juzi na jana.Na bahati nzuri Rais Samia amekuwa akisema mara kwa mara kuwa Tanznaia itajengwa na Watanzania , hakuna sababu ya kugawanyika.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...