Na Abdullatif Yunus MichuziTV.

Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka Mamlaka zinazohusika na Ukusanyaji wa Ushuru pamoja na Kodi mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba, kuacha Mara moja Ukusanyaji wa Kodi ya Miaka ya Nyuma kwa Wafanyabiashara hao kitendo kilichoonekana kuwaumiza kutokana na Ukubwa wa madeni.

Rais Samia ambaye yupo Mkoani Kagera kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Tatu, ameyasema Juni 9, 22 hayo wakati akihutubia Wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Uwanja wa Kaitaba, kufuatia ombi la Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wakili Stephen Byabato aliyewasilisha Kilio na manung'uniko ya Wafanyabiashara hao kuhusu kutozwa Kodi ya Miaka iliyopita.

"...Mhe. Rais Wafanyabiashara wamenituma na wanasema kiswahili unakijua, kwamba yaliyopita si ndwele, Miaka Mitano iliyopita CCM hatukuwa Madarakani katika Manispaa Yetu, hivyo Mhe Rais ikikupendeza uturuhusu Habari za Wafanyabiashara tuanzie hapa tulipo twende mbele haya Mambo yasitukwamishe katika Maendeleo yetu.." Amesema Mbunge Byabato ambaye ni Naibu Waziri wa Nishati.

Kufuatia Ombi hilo Rais Samia amesema kuwa Mamlaka zinatakiwa kukusanya Kodi kuanzia Mwaka mmoja nyuma na kwamba hiyo Miaka mingine ni uzembe wa waliokuwa Madarakani.


"...Nataka kusema hivi, Miaka yote hiyo watoza Kodi wapo, Halmashauri zipo, mmewaachia watu (Wafanyabiashara) Kodi hawakulipa, Leo hii unampelekea bill ya Miaka Mitano Sita nyuma alipe Nini? Wakati ule ulikuwa wapi? Kama hakulipa ndio ni Kosa lakini kosa sio lake pekee hata wewe ambaye hukumfuata kuikusanya, kwahiyo kama alivyosema Mbunge achaneni na hiyo Biashara, mnaloweza kufanya ni kurudi Mwaka mmoja nyuma..." Amesema Rais Samia.

Sambamba na hilo Mhe. Rais Samia amemuahidi Mbunge Byabato na Wanakagera hususani Wanabukoba Mjini kuwa Mkoa Kagera kwa Sasa utapewa kipaumbele katika Utekelezaji wa Miradi iliyokwama ikiwemo Ujenzi wa Stendi mpya, Soko la Kisasa, Taa za Barabarani, Machinjio ya Kisasa na Ujenzi wa Kingo za Mto Kanoni ili kuhakikikisha wanamaliza kero hizo.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...