Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewataka wasomi na wataalamu wa afya nchini kujikita katika tafiti zinazoendana na maendeleo ya teknolojia ili kuwa na mfumo wa afya utakaokuwa tayari kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama Uviko19.
Dkt. Mollel ametoa rai hiyo leo katika mkutano wa kisayansi uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko, amesema janga la Uviko19 lilipokumba ulimwengu ilidhihirisha udhaifu katika sekta za afya ulimwenguni kwani janga hilo lilionekana kshamiri na kushindwa kudhibitika.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wataalamu wa chuo wameeleza umuhimu wa nchi kuimarisha utendaji wa mfumo wa afya na uthabiti katika kukabiliana na dharura za afya ya umma.
Aidha Dkt. Mollel ametoa wito kwa wasomi wa vyuo vikuu nchini katika sekta ya afya kutumia taaluma zao kuja na suluhu la matatizo yanyoikumba sekta ya Afya badala ya kuwa walalamikaji kwa serikali.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wataalamu wa chuo wameeleza umuhimu wa nchi kuimarisha utendaji wa mfumo wa afya na uthabiti katika kukabiliana na dharura za afya ya umma.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof.Yohana Mashalla amesema magonjwa ya kuambukiza yamekuwa changamoto kubwa sana kwa nchi zinazoendelea kulinganisha na zile zilizoendelea.
Amesema mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 umeonesha ni kwa namna gani taifa linapaswa kuweka mifumo imara kujiandaa kukabiliana na majanga ya aina hiyo yatakapotokea siku za mbele.
“Iko haja ya kuimarisha mifumo yetu ya afya ili tuweze kujitayarisha kukabiliana na maradhi ya mlipuko kama COVID 19 na lazima tufahamu kuwa COVID siyo ya kwanza na wala siyo ya mwisho kuna milipuko itakuja tujiandae,” Amesema
Nae rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Bw.Nimrod Matungwa amesema mkutano huo utakwenda kuwa chachu ya ufumbuzi zaidi kwa namna ambavyo wanaweza kukabiliana na janga la Covid-19 pamoja na matatizo ambayo yanatokea kwenye sekta ya Afya.

Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akipokea cheti cha heshima na shukurani kwa niaba ya Wizara ya Afya kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof.Yohana Mashalla kwa ushiriki mkubwa katika mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG.

Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akimkabidhi cheti cha shukurani kutoka kwa Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe.Tri Yogo Jatmiko kwa ushriki wake mkubwa kwenye Kongamano hilo.


Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.



Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akizungumza na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki mara baada ya kuwasili katika mkutano wa kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.Pichani kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof.Yohana Mashalla


Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe.Tri Yogo Jatmiko (katikati) akijitambulisha na kuzungumza Mbele ya Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel pamoja na Uongozi wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki kabla ya kwenda kwenye mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Bi.Kokushubila Kairuki akizungumza katika mkutano wa kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof.Yohana Mashalla akizungumza katika mkutano wa kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe.Tri Yogo Jatmiko akizungumza jambo kwenye mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akimpa mkono wa Pongezi kwa ushiriki wa Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe.Tri Yogo Jatmiko kwenye Kongamano hilo.




Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya pamoja na wadau wa Afya wakiwa katika mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akizungumza katika mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Sehemu ya Uongozi wa Taasisi ya Ongea na Mwanao wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo katika mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...