Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshuhudia Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana wakibadilishana Mkataba wa Makubaliano kwenye masuala ya Utalii kupitia Wizara ya Urithi na Utalii ya Oman (kwenye Sekta ya Utalii) ya nchi hiyo katika hafla iliyofanyika Al Bustan, Muscat nchini Oman tarehe 13 Juni, 2022.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshuhudia Waziri wa Nishati January Makamba wakati akiweka Saini Mkataba wa Makubaliano kwenye masuala ya Nishati (Oil and Gas) kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Oman kupitia Wizara ya Nishati na Madini (Sekta ya Madini) ya nchi hiyo katika hafla iliyofanyika Al Bustan, Muscat nchini Oman tarehe 13 Juni, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshuhudia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiweka Saini Mkataba wa Makubaliano kwenye Sekta ya Elimu ya Juu pamoja na Serikali ya Oman katika hafla iliyofanyika Al Bustan, Muscat nchini Oman tarehe 13 Juni, 2022.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Shariff Ali Shariff akisaini Mkataba wa Makubaliano pamoja na Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Oman (OIA) kuhusu Mashirikiano ya kutangaza Uwekezaji baina ya nchi mbili kushirikiana katika kupata uzoefu na kusaidiana katika uwezeshaji wa kiteknolojia na Mafunzo iliyowakilishwa Naibu Mtendaji Mkuu wa (OIA) Mulham Basheer Al Jaraf tarehe 13 Juni, 2022.

Mkataba wa Makubaliano katika ya Jumuiya ya Watoa huduma katika Sekta ya mafuta na Gesi (AGAS) na Jumuiya ya watoa huduma katika sekta ya mafuta na gesi Zanzibar ZAOGAS pamoja na Jumuiya ya watoa huduma za Mafuta kutoka Oman (OPAL) katika hafla iliyofanyika Muscat Oman Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Biashara ya Zanzibar Ali Amour katikati ni Mwenyekiti wa ATOG Balozi Abdulsamad Abdulrahim na kwa upande wa Oman ni Mkurugenzi Mtendaji wa OPAL Abdulrahman Al Yahya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...