- Akabidhi kiasi Cha Shilingi Milioni 5,310,000 kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi ya kumpatia mtaji wa Biashara na fedha za kujikimu Ndg. Yassin Said mwenye Ulemavu wa Ngozi aliemuandikia barua Rais akiomba kuwezeshwa kiuchumi Baada ya kupitia masaibu katika maisha yake.
Akikabidhi fedha hizo kwa niaba ya Rais Samia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemsisitiza Kijana Yassin kutumia fedha alizopatiwa kujiimarisha kiuchumi ili lengo la Rais kutoa fedha hizo liweze kutimia.
Kwa upande wake Ndg. Yassin Said amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada aliopatiwa na kuahidi kuzitumia kwa lengo lililokusudiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...