Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, ameitaka Taasisi ya Teknolojia Dar es saalam (DIT) kupitia kampuni yake tanzu kusajili bunifu zake ili kuzilinda dhidi ya watu ambao wamekuwa na tabia ya kuiba bunifu.

Mtaka ameyasema hayo leo Juni 14,2022  jijini Dodoma wakati wa Maonyesho ya bunifu mbalimbali zilizofanywa na taasisi hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Mtaka, amesema kuwa  kumekuwepo na watu ambao wamekuwa wazuri katika kuiba bunifu za watu wengine hivyo kama taasisi hiyo haiatakuwa makini inaweza kujikuta katika wakati mgumu.

“Ni wapaongeze kwa bunifu mnazofanya lakini mnapaswa kuzisajili na kuanza kuzifanyia kazi au kuziuza kwani hizo bunifu ni fedha hamna  sababu ya kuendelea kulalamika wakati mmekaa na bunifu kama hizi kwenye makabati”amesema

 Mtaka ameichagua taasisi hiyo kufanya kazi kwa wafanyakazi wa bodaboda kwa kutembelea baadhi ya wilaya zilizopo Mkoani humo.

Amesema DIT inauwezo mkubwa katika ufanyaji wa kazi zake na imezalisha wabunifu wengi katika bunifu mbalimbali.

“Mnauwezo mkubwa na ndio maana leo tumewachagua kufanya kazi na Dodoma ambapo kesho mtaanza kuwasajili wanaofanya kazi ya bodaboda”,Amesema Mtaka

“Ubunifu huu umekuwa wa kipekee sana na tunataka tuone mkiendelea kubuni bunifu mbalimbali ambazo nchi nyingine zitaiga kutoka kwetu”

Hata hivyo amewataka wakuu wa wilaya za Dodoma kuitumia taasisi hiyo ili kupata mifumo mbalimbali itayo wasaidia kujibu kero mbalimbali katika maeneo yao.

Meneja Masoko kampuni ya DIT, Agnes Kimwaga,amesema kuwa Taasisi hiyo  imeaanza kubiasharailisha bunifu mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na wanafunzi wake ili kwenda kujibu changamoto zilizopo katika jamii.

“Kampuni hii itaweza kuuza bunifu zote ambazo zimefanywa kwa kuzipeleka sokoni na kuziuza badala ya kubaki katika makabati bila kuwa na tija”amesema Kimwaga

Aidha amesema kuwa kabla ya kuanzishwa kampuni hiyo tanzu bunifu nyingi zilikuwa zinabaki na kufungiwa kwenye makabati ofisini bili kuwa na manufaa kwa taasisi na jamii.

“Tumekuwa tukiandaa bunifu mbalimbali kupitia wanafunzi wetu lakini zinaishia kwenye makabati sasa tumeamua kuzibiasharailisha bunifu zote ili kwenda kujibu changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii”amefafanua Kimwaga 

Hata hivyo Kimwaga amemshukuru Mtaka kwa kuwa tayari kufanya kazi pamoja na DIT

“Tunamshukuru Sana Mhe.Mtaka kwa kuwa tayari kufanya kazi pamoja na sisi na kesho tunaanza na hiyo ya bodaboda ambayo imetengenezwa na Dkt.Budoya

“Na kikubwa zaidi tumekaribishwa kila wilaya na sisi tutaenda kila wilaya ambazo tumekaribishwa na tutafika pia mpaka ngazi ya kata na tutakuwa tumefanya kazi kubwa”.Amesema Kimwaga

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa Maonyesho ya bunifu mbalimbali zilizofanywa na Taasisi ya Teknolojia Dar es saalam (DIT) kupitia kampuni yake tanzu yaliyofanyika leo Juni 14,2022 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dk Fatma Maganga,akizungumza wakati wa Maonyesho ya bunifu mbalimbali zilizofanywa na Taasisi ya Teknolojia Dar es saalam (DIT) kupitia kampuni yake tanzu yaliyofanyika leo Juni 14,2022 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafunzo wanayotoa katika taasisi hiyo na umuhimu wa ushiriki katika uchumi wa viwanda leo jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko kampuni ya DIT, Agnes Kimwaga,akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kuwapa nafasi ya kuonyesha bunifu zao katika ofisi zake jijini Dodoma.


Sehemu ya Viongozi pamoja na washiriki wakifatilia hotuba ya Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka (hayupo pichani)wakati wa Maonyesho ya bunifu mbalimbali zilizofanywa na Taasisi ya Teknolojia Dar es saalam (DIT) kupitia kampuni yake tanzu yaliyofanyika leo Juni 14,2022 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...