Na Ripota Wetu, Simiyu
WAKULIMA katika mkoa wa Simiyu watafaidika na ujio wa Pembejeo za Kilimo na Dawa baada ya Serikali ya Tanzania kutoa ahadi hiyo ya Pembejeo hizo bure kwa Wakulima hao hususani Wakulima wa zao la Pamba.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo katika Mkutano wa Chama hicho Wilayani Maswa Mkoani Simiyu, amesema Serikali imedhamiria kutatua changamoto ya upatikanaji wa Pembejeo kwa Wakulima hao ili kuwaongezea tija katika uzalishaji wa mazao bora.
“Tunaenda kukaa na Wizara ya Kilimo, tunaenda kuweka msukumo kuhakikisha msimu ujao Wakulima wa Simiyu mnapata Pembejeo na Dawa mbalimbali za mazao yenu, na Pembejeo zinazoendana na mahitaji yenu kama Wakulima”, amesema Chongolo.
Amesema Pembejeo hizo zitatolewa bure bila malipo kwa Wakulima hao, amewaasa kuepuka Walanguzi wa Pembejeo ambao watataka kutoa Pembejeo hizo kwa malipo, “Pembejeo zinazolewa kwenu kama Wakulima ni bure, bila malipo atayejitokeza na kutaka kuuza kwenu huyo atakuwa Mlanguzi na atakuwa Mhujumu Uchumi”, ameeleza Chongolo.
Pia ameupongeza Mkoa huo kwa Kilimo bora cha zao la Pamba, akitaja zao hilo ni Dhahabu nyeupe, pia amewataka kulima zao hilo kwa nidhamu na kupata mavuno ya kutosha na kujipatia fedha ya uhakika katika mauzo.
“Kwa sasa hivi kuna uhakika wa kuuza zao la Pamba, KG 1 hadi Tsh. 2000/-, kutoka awali kwenye bei tofauti za Tsh. 1050, Tsh. 1560, Tsh. 1700, Tsh. 1800, na sasa hivi Soko la uhakika lina patikana”, amesema Chongolo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...