Viongozi,Watendaji na Maafisa Waandamizi wa Serikali wamekutana na kufanya mazungumzo na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya China inayotarajia kuwekeza katika kilimo cha soya nchini. Mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ofisi ya Wizara ya Kilimo jijini Dodoma yalilenga kujadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza katika mkutano huo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa Serikali inashauku kubwa kuona uwekezaji huu ambao unaenda kuwainua wakulima wadogo kiuchumi, unaanza kutekelezwa mapema iwezekanavyo. Naibu Waziri mavunde aliongeza kuwa kwa upande wa serikali tayari imeshaweka mazingira mazuri na rafiki ya kuhakikisha kuwa mradi huu unatekelezwa kwa mafanikio nchini.

“Pamoja na mambo mengi muhimu tuliyofanya ili kuharakisha uwekezaji huu wa kuongeza uzalishaji na ubora wa soya nchini, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kuanzia imetenga takriban hekari 27000 ambazo zitatumika katika uzalishaji wa mbegu za soya” Alisema Naibu Waziri Mavunde.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Longping High Tech Bw. Liang Shi ameeleza kuwa baada ya ziara waliyoifanya katika maeneo mbalimbali nchini wamepata mwamko zaidi wa kuanza uwekezaji haraka iwezekavyo.

“Katika kipindi tulichokuwepo hapa nchini tumetembelea maeneo mbalimbali tumeona ardhi na hali ya hewa nzuri kwa uzalishaji wa soya, utayari wa wakulima na zaidi utayari wa Serikali katika kupokea uwekezaji wetu ambao pamoja masuala mengine unatoa uhakika wa soko la soya za wakulima. Tumefarijika na kuhamasika zaidi hivyo tuna ahidi uwekezaji wetu utaanza mara moja”. Amesema Bw. Shangyang Wu

Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech wamekuwepo nchini kwa kipindi cha takribani wiki mbili ambapo wametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Ruvuma, Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa na Katavi kwa lengo la kuangalia maeneo ya uzalishaji wa soya sambamba na kuonana na kufanya mazunguzmo na wadau katika sekta hiyo. 



Viongozi,Watendaji, Maafisa Waandamizi wa Serikali, wadau kutoka sekta binafsi na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya nchina China wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano uliofanyika katika ofisi ya Wizara ya Kilimo jijini Dodoma

Viongozi,Watendaji, Maafisa Waandamizi wa Serikali, wadau kutoka sekta binafsi na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya nchina China wakiwa kenye mkutano

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Antony Mavunde akizungumza wakati wa kikao baina  ya Viongozi,Watendaji na Maafisa Waandamizi wa Serikali na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya China kilichofanyika katika ofisi ya Wizara hiyo jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...