KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameshiriki kwenye tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa Kada ya Chama hicho wilayani Nachingwea Ramadhan Mwarabu Mmoro aliyefariki dunia Mei 31 mwaka huu.
Kada huyo wa CCM aliyezaliwa mwaka 1979 enzi za uhai wake ameshiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa Chama hicho kwa kushika nafasi mbalimbali za ngzi ya kata pamoja na kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Nachingwea. Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya Nachingwea(NAFA).
Akizungumza mbele ya waombolezaji walioshiriki kwenye kuaga mwili wa kada huyo, Shaka ametoa pole kwa msiba huo mzito ambao umewakuta ndugu, jamaa na marafiki huku akitoa rai kwa waombolezaji kumuombea marehemu ili Mungu amuepushe na adhabu za kaburini.
“Tumekuja kuwafariji wenzetu, safari hii ni yetu sote kinachotokea tunapishana muda wa nani ameanza na nani anafuata.Dini zote zinasema kufa ni haki kwa kiumbe waliombwa na Mwenyezi Mungu.Hata hivyo ni vema tukatiana moyo kwenye matatizo.
“Niwaombe ndugu zetu ambao wameguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira. Kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia anatoa pole kwa msiba huu,’amesema Shaka alipokuwa akizungumza mbele ya waombolezaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...