HALMASHAURI ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imepata hati safi (Unqualified Opinion) kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Pia
Halmashauri hiyo imefunga hoja 31 kati ya hoja 41 baada ya mdhibiti na
mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali CAG kuhakiki na kuridhia majibu
yaliyowasilishwa na kufanya hoja zisizofungwa kuwa 10.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Samwel Warioba
ameyasema hayo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa
ya CAG ya mwaka 2020/2021.
Warioba
amesema kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 na vipindi vya nyuma
halmashauri ilikuwa na jumla ya hoja 41 na hoja 24 ziliibuliwa na
kutolewa mapendekezo katika mwaka 2020/2021 pekee.
Hata
hivyo, amesema hoja nne za mwaka 2020/2021 na hoja sita za miaka ya
nyuma, mkaguzi hajaridhia kuzifunga kutokana na baadhi ya hizo kuwa za
kimfumo na kiutendaji.
"Kwa
miaka ya nyuma hoja ambazo CAG alikuwa hajaridhia kuzifunga ni 17
ikihusisha hoja za miaka ya kuanzia 2014/2015 hadi 2019/2020," amesema
Warioba.
Amesema jumla ya
hoja 10 ambazo hazijafungwa, utekelezaji wa hoja zilizobaki unaendelea
kwa matarajio kuwa zitafanyiwa ufumbuzi baada ya kikao na majibu na
vielelezo vyake vitawasilishwa kwa wakaguzi mwakani.
"Ofisi
ya mkurugenzi inapenda kutoa shukurani za dhati kwa Mwenyekiti wa
halmashauri, mbunge na madiwani kwa uratibu, ushauri na maelekezo ya
mara kwa mara hadi ofisi ya CAG kutoa hati safi," amesema Warioba.
Mkuu
wa mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere, pamoja na kuwapongeza
kwa kupata hati safi ameiagiza halmashauri hiyo kumaliza hoja 11
zilizopo.
Mkuu wa Wilaya
ya Simanjiro Dk Suleiman Serera, amesema kasoro ndogo ndogo
zilizojitokeza zinapaswa kumalizwa Kwa utaratibu maalum.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...