Kutoka Paris,Ufaransa

Taasisi ya Suzan Thompson Buffet Foundation (STBF) yenye Makao Makuu yake nchini Marekani imekubali kutoa msaada wa dola za Kimarekeni milioni 15 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 34.5 kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya ya Uzazi ,Mama na Mtoto kwa kipindi cha miaka mitatu.

Hayo yamebainishwa katika mazungumzo yao baina ya Waziri wa Afya, Mhe Ummy Mwalimu na Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Senait Fisseha katika kikao cha 14 cha Wafadhili wa Afya ya Mama, Mtoto na Vijana (Global Financing Facility for Women Children and Adolescent Health) Jijini Paris.

Waziri Ummy amesema fedha hizo zitasaidia kuimarisha utoaji wa huduma za afya ya uzazi ikiwemo kuhakikisha kuwa watoa huduma wa afya ngazi ya msingi ya jamii wanapatikana wa kutosha.

Aidha, Waziri Ummy amemshukuru Prof. Senait na kuahidi kuwa fedha hizo zitasimamiwa kikamilifu ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa ya kuokoa maisha ya wanawake, watoto na vijana.

Ameongeza kuwa fedha hizo zitaelekezwa kuimarisha utoaji wa huduma kwenye vituo vya kutolea huduma ikiwemo huduma rafiki kwa vijana.

Naye, Prof. Senait amesema ameiona dhamira njema ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha huduma za afya ya Uzazi, Mama na Mtoto hivyo wapo tayari kumuunga mkono ili aweze kutimiza vyema maono yake

Hivyo Taasisi ya STBF imeonesha nia ya kuongeza fedha zaidi kwa Tanzania endapo utekelezaji wa msaada huo utakuwa wa mafanikio. 

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji wa STBF Prof. Senait Fisseha

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtendaji wa SBTF Prof. Senait Fisseh.Kulia kwa Waziri Ummy ni Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Afya ya Uzazi,Mama na Mtoto(Wizara ya Afya) Dkt. Ahmad Makuwani na mwisho kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Beatrice Mutayoba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...