Matukio mbalimbali Pichani yakimuonesha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wakati akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo la Migori mkoani Iringa leo tarehe 09/06/2022 ambapo amewataka kuachana na vitendo vya mauaji yanayotokana na wivu wa mapenzi sambamba na kuwataka waendesha pikipiki maarufu bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani. Picha na Demetrius Njimbwi Jeshi la Polisi.

………………………………………..

IRINGA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameendelea kukemea na kulaani vitendo vya mauaji vinavyotokana na wivu wa mapenzi ambavyo vimekuwa vikitekelezwa na baadhi ya watu kwenye jamii jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.

IGP Sirro amesema hayo akiwa na eneo la Migori mkoani Iringa wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo.

Kuhusu ajali zinazotokana na Pikipiki IGP Sirro amewataka watumiaji wa vyombo hivyo kufuata kanuni na sheria za usalama barabarani na kuhakikisha wanavaa kofia ngumu.

Kuhusu Panya Road IGP Sirro amesema kuwa, jeshi la Polisi limeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kudhibiti kundi hilo na kuitaka jamii kuhakikisha inaimarisha maelezi ya familia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...