Meneja Tathmni na Ufatiliaji wa Miradi Rahma Musoke wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation akifafnua miradi iliyofanywa na taasisi yao tangu kufariki dunia kwa Hayati  Rais Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya - Senkoro na wakwanza kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Uongozi wa Mkapa katika Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Rita Kahurananga.


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
TAASISI ya Benjamin William Mkapa, Julai 13 na 14, 2022 visiwani Zanzibar inatarajiwa kufanya Kongamano la pili la kumbukizi ya Muasisi wa Taasisi hiyo, Aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu nchini Tanzania, Hayati Benjamin Mkapa, Kongamano hilo likiwa na Kaulimbiu ya ‘Uongozi Madhubuti Hamasa ya Mabadiliko kwa Wote’.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro amesema jukwaa hilo litajadili mada kuu mbili ambazo ni kuongeza kasi katika mikakati ya mabadiliko katika mifumo ya Afya nchini Tanzania kupitia biashara ushirika.

Dkt. Ellen amesema mada nyingine ni ubunifu katika miradi na mikakati ya ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi za Umma na Sekta Binafsi katika kuleta huduma bora za Afya kwa wote.

“Kupitia mada hizo, Washiriki watapata fursa ya kusikia mijadala ya juhudi za mashirikiano ya Serikali za Tanzania Bara na Visiwani, Sekta Binafsi na wadau wa maendeleo na kuchagizwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa, katika kuimarisha mifumo ya Afya kwa lengo la kuhakikisha kila mtu anapata fursa kupata huduma bora za afya”, amesema Dkt. Senkoro.

Amesema takribani Wageni 500 wanatarajiwa kushiriki huku siku ya kwanza mdahalo ukifunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Othman Masoud na siku ya pili, Julai 14, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa rasmi huku mdahalo huo ukihudhuriwa na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye ni Msarifu wa Taasisi hiyo.

Kwa upande wake, Meneja wa Usimamizi na Tathimini na Ufuatiliaji wa Miradi ya Taasisi hiyo, Rahma Musoke amesema hadi sasa kupitia ‘Program’ zake Taasisi ya Benjamin Mkapa imefika watu Milioni 26 kupitia Miradi yake mbalimbali kwenye Mikoa yote ya Tanzania.

Rahma amesema Miradi hiyo inalenga makundi tofauti katika kuboresha utoaji huduma za Afya, hata hivyo katika Sekta ya Afya wamepeleka Watumishi katika vituo mbalimbali kupitia wadau wa maendeleo na michango ambayo inapatikana sanjari na kuajiri Watumishi na kuwapeleka katika maeneo mbalimbali.

“Watumishi zaidi ya 10,042 tumewaajiri hadi sasa na kuwapeleka katika vituo mbalimbali kutoa huduma za Afya, ambao wapo kwenye maeneo ya Vijijini ni 5882 na wengine wanatoa huduma katika ngazi ya vituo”, amesema Musoke.

Amesema hadi sasa Watumishi asilimia 80% wameajiriwa kwenye mifumo ya ajira Serikalini, pia Taasisi hiyo imeboresha miundombinu kwa ujenzi wa Nyumba za Watumishi ili waendelee kukaa kwenye makazi bora na kutoa huduma bora za Afya kwa Jamii.

“Tumejenga Nyumba za Watumishi 482 ambao wanaajiriwa katika mikoa mbalimbali nchini, maeneo ambayo ni magumu kufikika kwa urahisi, tumeboresha miundombinu ya vituo vya Afya 268 kwa ujumla vituo vya Afya 537 vimefanyiwa marekebisho kutoa huduma nzuri”, ameeleza.

“Tumetoa Udhamini wa Masomo (Scholarships) kwa Wanafunzi wa kada mbalimbali za Afya katika vituo vya kutoa elimu ya Afya, Taasisi ya Benjamin Mkapa imetoa udhamini huo kwa Wanafunzi 933 na wamenufaika kupitia miradi hiyo”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...