Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi kuwa inashiriki maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika Uwanja wa Maonyesho wa Biashara wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28/06/2022 hadi tarehe 13/07/2022.

Katika maonesho haya JKCI inafanya upimaji wa afya ya moyo kwa watoto na watu wazima. Pia inatoa chanjo ya UVIKO-19 kama kinga ya ugonjwa huu pamoja na kufanya kipimo cha kuchunguza UVIKO -19 (rapid test) kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo katika njia ya kupumulia.

Taasisi hiyo pia ina wataalamu wa lishe ambao wanatoa elimu ya lishe bora ambayo inawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo na kisukari ambayo ni magonjwa yasiyoambukiza na mtu anaweza kuyaepuka kwa kufuata ushauri wa kitaalamu wa lishe.

Kwa wale watakaokutwa na matatizo ya moyo watapatiwa matibabu hii ikiwa ni pamoja na kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.

Madaktari mabingwa wa magonjwa ya moyo wa JKCI ya kina Peter Kisenge, Tulizo Shem, Tatizo Waane, Baraka Ndelwa na Pedro Pallangyo chini ya uongozi wa Prof. Mohamed Janabi watakuwepo katika banda letu kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi. Nyote mnakaribishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...