Tanesco mkoani Kagera yatumia ipasavyo siku ya Uzinduzi wa Filamu ya ROYAL TOUR kimkoa uliofanywa na Mkuu wa Mkoa KAGERA Mhe Meja Jenerali Charles Mbuge Kutangaza MFUMO mpya wa utoaji huduma kwa njia ya mtandao, Unaotambulika kama NIKONEKT.
Viongozi mbalimbali wa Wilaya na Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa pamoja na Wakazi wa BUKOBA waliohudhuria Tukio hilo wamejulishwa Utaratibu wa kupata huduma za TANESCO/UMEME kwa kupitia mfumo wa NIKONEKT.
NIKONEKT Ni mfumo mpya wa utoaji huduma wa TANESCO unaowezesha waombaji huduma kufanya maombi yao kimtandao kwa kutumia NIKONEKT APP ufumo huu unatarajiwa kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa kumuwezesha mteja kuomba UMEME na KULIPIA mtandaoni Hadi Kuunganishiwa UMEME bila Kufika Ofisi za TANESCO.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO KAGERA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...