Njombe

Ili kurahisisha huduma ya maombi ya umeme,shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limeanzisha na kuzindua huduma mpya ya maombi ya kuunganishiwa nishati ya umeme kupitia simu zao.

Akizungumza mara baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo inayoitwa Ni-Konekt iliyofanyika katika viwanja vya polisi mjini Makambako mkoani Njombe,Zaidat Ngoda afisa uhusiano wa huduma kwa wateja kutoka TANESCO Makambako amesema huduma hiyo inakwenda kuwaondolea usumbufu wananchi kufika ofisini kwa ajili ya maombi ya umeme.

“Kupitia huduma hii mteja anapata huduma ya umeme popote pale alipo na hii huduma inapatikana kwa njia nne kwa kumuangalia mwananchi yeyote mpaka mwenye simu ndogo aweze kufanya maombi ya kuunganishiwa uememe lakini njia nyinge ni ya kupitia tovuti ya  WWW.TANESCO.CO.TZ”  alisema Zaidat Ngoda

Amesema ili kupata huduma hiyo kupitia simu ndogo ya kiganjani (kiswaswadu) mteja ataweza kupata huduma hiyo kwa kwa kubonya *152* 00 na kasha alama ya reli na kuendelea kufuata maelekezo huku kwa watumiaji wa simu janja wataweza kupakua application inayoitwa Ni-Konekt ambayo ina maelezo ndani ya maombi ya huduma ya umeme.

Nolasco Mlowe ni diwani wa kata ya mji mwema aliyefika katika uzinduzi wa huduma hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako,amesema mfumo huo utawasaidia sana wananchi kwa kuwa awali walikuwa wakipata taabu ya kufuatilia ofisi za TANESCO badala ya kuendelea na shughuli zao.

“Awali kulikuwa na hatua nyingi mpaka kwenda kwenye ofisi zao tu na mizunguko mingine mingi lakini mfumo huu unaweza ukalipia kila kitu ukiwa nyumbani kwako na kufungiwa umeme hivyo unapunguza muda nan i mfumo salama zaidi wa kuepukana na matapeli”Amesema Mlowe

Aidha ametoa wito kwa TANESCO kuendelea kutoa elimu kwa shirika la umeme ili huduma hiyo iweze kuwafikia wananchi.

Nao baadhi ya wananchi wa Makambako waliojitokeza katika hafla hiyo wamepongeza shirika la Umeme kwa kuendelea kuwajali na kuzidi kuwarahisishia huduma




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...