Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Ndg. John M. Mnali katika kuhakikisha maboresho ya huduma kwa wawekezaji hasa kwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) unafanikiwa, wamesaini makubaliano ya awali ya mashirikiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kutumia mfumo wa pamoja ambao utawezesha huduma wanazotoa NIDA na TIC kwa wawekezaji kuweza kusomana/kuonekana kwenye mfumo mmoja.


Hafla hiyo fupi imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa TIC uliopo mtaa wa Shaban Robert jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Juni, 2022.

Tasisi 12 za Serikali zinazotoa huduma kwa wawekezaji zimekubaliana kusaini mikataba ya mashirikiano ya awali ili kutumia mfumo mmoja wa huduma Kwa wakezaji katika kuhakikisha Wawekezaji wanapata huduma zote Kwa urahisi na haraka. NIDA na TIC tayari wamesaini makubaliano hayo taasisi zingine ambazo bado zitakamilisha suala hilo kabla ya tarehe 15 Juni, 2022.

Kituo cha uwekezaji Tanzania kinafanya kazi pamoja na taasisi kumi na mbili za Serikali zinazotoa huduma mahala pamoja (NIFC ) taasisi hizo ni BRELA, NEMC, NIDA, TRA, UHAMIAJI, ARDHI, KAMISHINA WA KAZI, TANESCO, OSHA, TBS na TMDA.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Ndg. John Mnali (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Usajili kutoka NIDA Ndugu Edson Guyai (kulia) Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu NIDA, wamesaini mikataba ya ushirikiano ya huduma ya pamoja kwa wawekezaji katika kumbi wa TIC uliopo mtaa wa Shaban Robert jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Ndg. John Mnali (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Usajili kutoka NIDA Ndugu Edson Guyai (kulia), kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu NIDA wakionesha nakala za mikataba ya mashirikiano ya huduma ya pamoja Kwa wawekezaji iliyosainiwa Leo na Tasisi hizo ili kuanza utekelezaji.
Pichani ni wafanyakazi wa TIC na wafanyakazi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali waliohudhuria katika kusaini mikataba ya mashirikiano ya Huduma Kwa Wawekezaji iliyoongozwa na Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa TIC Ndugu John Mnali  kwenye Ukumbi wa kituo Cha uwekezaji uliopo mtaa wa Shaban Robert jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Wizara ya Ardhi TIC Ndg. Jonas Chikawe akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya mashirikiano ya Huduma ya pamoja kwa wawekezaji kati Wizara ya Ardhi na TIC uliofanywa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Ndg. John Mnali kwenye ukumbi wa kituo cha uwekezaji Tanzania Leo tarehe 10 June 2022.
Baadhi Wakurugenzi na Viongozi mbalimbali kutoka Tasisi za serikali wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukamilisha zoezi la utiaji saini wa mikataba ya mashirikiano ya huduma ya pamoja wa wawekezaji katika kituo cha uwekezaji Tanzania leo tarehe 10 June 2022.
Baadhi ya wafanyakazi wa TIC wakishuhudia utiaji Saini wa mikataba ya mashirikiano ya huduma ya pamoja Kwa Wawekezaji kati ya TIC na NIDA kwenye Ukumbi wa kituo cha uwekezaji Tanzania leo tarehe 10 June 2022.



 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...