Na Bakari Madjeshi, Michuzi Blog

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili imethibitisha kuwa Msanii na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule maarufu kwa jina la Prof. Jay ameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya afya yake kuimarika ikiwa ni siku 127 tangu afike katika Hospitali hiyo kwa matibabu.

Muhimbili wamethibitisha taarifa hiyo kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, katika Hospitali hiyo, Aminieli Eligaeshi sanjari na majukwaa ya mitandao ya kijamii, kuhusu taarifa hiyo ya kuruhusiwa Msanii huyo wa Hip Hop nchini.

“Msanii Joseph Haule (Prof. J) jana ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu kwa siku 127 na afya yake kuimarika”, taarifa hiyo imeeleza ikiambatana na chapisho la picha ya Msanii huyo akiwa kwenye sura ya furaha.

Pia kupitia Vyombo vya Habari, Familia ya Msanii huyo imethibitisha kurejea nyumbani kwa Prof Jay ikiwa ni siku 127 tangu afikishwe Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu, pia Familia hiyo imeeleza kuwa afya yake imeimarika vizuri, huku wakibainisha kuwa anaongea na atambua watu vizuri endapo ataonana nao.

“Hadi sasa anaongea vizuri tu, na akili yake ipo vizuri asilimia 100%, akili yake inatambua vizuzi tu! hasahau chochote ikiwa kuna watu ambao anawafahamu, hata tukimtajia watu hao, anasema anawafahamu na kuwakumbuka vizuri bila shida yoyote, kwa sasa tunajitahidi kumuweka awe imara kutokana na kulala Kitandani muda mrefu”, amesema Mke wake, (Prof Jay) Grace Mgonjo

Hata hivyo, Familia hiyo imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu pamoja na Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mchango wao katika kipindi chote hadi kufanikisha kuimarika afya ya Prof Jay.

Sisi tunawashukuru watu wote waliokuwa nasi bega kwa bega katika kipindi chote cha kuuguza, tunawashukuru wote kwa kutuombea pia, Chama cha CCM, CHADEMA, na wengine wote waliokuwa kwenye tasnia yake ya Muziki na hata wale wasiokuwa kwenye tasnia hiyo”, imeeleza Familia hiyo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...