Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

MANISPAA ya Ubungo imeadhimisha siku ya mtoto wa Afrika katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Young Counseling Organization ( YOCO) kilochopo Malamba Mawili kwa kutoa Elimu kwa wanafunzi 120 kutoka katika shule za sekondari na msingi zilizopo katika Wilaya hiyo.

Maadhimisho hayo yameenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Tuimarishe ulinzi wa mtoto; tokomeza ukatili dhidi yake” tujiandae kuhesabiwa.

Akiongea Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Hanan Mohammed Bafagil amewaasa wanafunzi kuhakikisha wanapopata changamoto za ukatili wa kijinsia, manyanyaso katika familia na hata mashuleni kuwasilisha kwa wazazi au walimu wao na kuwataka Kufika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ili waweze kupatiwa ufumbuzi.

“Serikali yetu ni sikivu na viongozi wako makini , tunaahidi kutoa ushirikiano bega kwa bega kila mwenye jambo linalomtatiza alifikishe mahali panapostahili ni lazima litafanyiwa kazi” Hanan aliendelea kusisitiza.

Alikadhalika amewashukuru wadau wa Asas mbalimbali walioshiriki katika baraza la watoto wakiwemo child intimacy,right sight organization, jamii safi salama, the chosen generation , crisis revolving center na n.k

Nae mratibu wa baraza la mtoto Manispaa ya Ubungo Bupe Mwansasu ameendelea kuzitaka Asas zilizoshiriki kuendelea kujitoa na kumshukuru Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha YOCO kwa kujitolea kutoa eneo lake kuanzia mwanzo hadi mwisho wa tukio.

Sambamba na hayo zoezi hilo limefanyika kwa kuwapa Elimu yakupambana na matukio ambayo yanawanyima haki zao za msingi, umuhimu wa kupata haki za watoto katika jamii, uongozi na uwajibikaji.

Aidha watoto wameelezea mahitaji yao ikiwemo kupata fursa yakusikilizwa, haki yakuendelezwa, haki yakuishi, haki kwa watoto wakike kupata nafasi yakushiriki michezo kama ilivyo kwa watoto wakiume na haki yakulindwa.

Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Hanan Mohammed Bafagil akizungumza na wanafunzi pamoja na watoto  yatima wa kituo cha yoco kilichopo Malamba mawili wakati wakuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika ambapo amewasihi watoto hao wanapopata changamoto za unyanyasaji wa kijinsia wawasilishe kwa wazazi au walezi wao.

Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Hanan Mohammed Bafagil ,Mratibu wa baraza la mtoto Manispaa ya Ubungo Bupe Mwansasu pamoja na viongozi wengine wakiwa na watoto wa shule za sekondari Malamba mawili na Msingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...