KAMPUNI inayoongoza kwa huduma za teknolojia na mawasiliano nchini imetunukiwa tuzo nne na Kampuni ya Serengeti bytes kupitia programu ya Tanzania Digital Awards.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo June 7, 2022 Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja, Harriet Lwakatare amesema kuwa Vodacomu Tanzania wamefurahia tuzo hizo na hiyo ndio inaonesha kazi kubwa unayofanywa na kampuni hiyo.
Amesema kuwa wametunukiwa tuzo nne (4) ambazo ni Tuzo ya Huduma bora kwa Mteja (best Customer care), ubunifu (Innovative telco of the Year), Mtoa huduma za Fedha kwa simu bora (Mobile Money, 'M-Pesa') pamoja na kampuni bora ya mawasiliano ya mwaka (Telco Company of the Year).
"Vodacom kama lengo letu lilivyo ni kutoa mawasiliano kwa wateja wetu wote tukitumia mbinu tofauti hasa ya kiteknolojia ya kisasa." Amesema Harriet
Amesema kuwa tuzo walizotunukiwa leo zinoanesha kwamba wanafikisha bidhaa na huduma iliyobora kwa mteja kwa kutumia teknolojia ya kidigitali ambapo ulimwengu umegeukia kwa sasa na wateja wameweza kutuonesha kwamba wanastahili tuzo hizo.
Amesema tuzo hizo zimetolewa kwa kura za wananchi... Kwahiyo tunashukuru sana wananchi wote hasa hasa wateja wetu wa Vodacom kwa kuendelea kutuamini kwa huduma zote bora tunazozitoa." Amesema Harriet
Mkurugenzi wa Huduma za kidijitali, Vodacom, Nguvu Kamando akipokea Tuzo kutoka kwa kampuni ya Serengeti Byttes kupitia programu ya Digital Awards anayemkabidhi tuzo ni Afisa uendeshaji Serengeti bytes, Michael Mallya. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Vodacom, Harriet Lwakatare.
Mkurugenzi wa Huduma za kidijitali, Vodacom, Nguvu Kamando akionesha Tuzo waliyoipata kutoka kwa kampuni ya Serengeti Byttes kupitia programu ya Digital Awards anayemkabidhi tuzo ni Afisa uendeshaji Serengeti bytes, Michael Mallya. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Vodacom, Harriet Lwakatare.
Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Vodacom, Harriet Lwakatare katika akipokea Tuzo kutoka kwa kampuni ya Serengeti Byttes kupitia programu ya Digital Awards anayemkabidhi tuzo ni Afisa uendeshaji Serengeti bytes, Michael Mallya. Kushoto Mkurugenzi wa Huduma za kidijitali, Vodacom, Nguvu Kamando.
Meneja wa Mpesa wa malipo ya kidijitali na Chaneli za Mtandaoni, Josephine Mushi akipokea Tuzo kutoka kwa kampuni ya Serengeti Byttes kupitia programu ya Digital Awards anayemkabidhi tuzo ni Afisa uendeshaji Serengeti bytes, Michael Mallya. kushoto ni Kaimu mkuu wa kitengo cha Mahudiano na Mawasiliano Vodacom, Christina Murimi
Kaimu mkuu wa kitengo cha Mahudiano na Mawasiliano Vodacom, Christina Murimi akipokea Tuzo kutoka kwa kampuni ya Serengeti Byttes kupitia programu ya Digital Awards anayemkabidhi tuzo ni Afisa uendeshaji Serengeti bytes, Michael Mallya. kushoto ni Meneja wa Mpesa wa malipo ya kidijitali na Chaneli za Mtandaoni, Josephine Mushi.
Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Vodacom, Harriet Lwakatare akizungumza na waandishi waa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 7, 2022 baada ya akipokea Tuzo kutoka kwa kampuni ya Serengeti Byttes kupitia programu ya Digital Awards.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...