* Balile ashauri kuwepo kwa sheria ya adhabu kwa kampuni zitakazoshindwa kulipa fedha za matangazo kwa vyombo vya habari 

WADAU wa sekta ya habari wameshauri waandishi wa habari kujiendeleza kielimu ili kuendelea kuiheshimisha tasnia hiyo pamoja na kujenga weledi, nidhamu na maadili kitaaluma na jamii kwa ujumla.

Hayo yameelezwa Juni 2 kupitia mkutano maalumu ulioandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania kwa waandishi wa habari na kujadili  Mapendekezo ya Mabadiiliko ya Sheria ya Habari nchini yaliyowasilishwa Serikalini.

Baadhi ya  waandishi wa habari walioshiriki mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao wameeleza kuwa suala na taaluma na vigezo vya tasnia hiyo ni vyema vikazingatiwa ili kuendelea kukuza weledi wa tasnia ya habari ambapo baadhi ya washiriki walieleza kuwa baadhi ya vyombo vya habari vikiwemo vituo vya Redio vimekuwa vikitumia watangazaji kwa vigezo vya vipaji na sio taaluma jambo linalodhoofisha tasnia ya habari.

Mmoja ya waandishi wa habari kutoka kituo cha Redio alieleza namna suala la elimu linavyopaswa kuzingatiwa na waandishi kutenga muda wa kujiendeleza ili kuendelea kuihudumia jamii kwa viwango vya juu pamoja na kuongeza maarifa katika utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia kanuni na sheria ya tasnia ya habari nchini.

Aidha mwanahabari kutoka kituo cha ITV Godfrey Monyo alieleza kuwa suala la elimu kwa waandishi wa habari litiliwe mkazo ili kuendelea kuboresha tasnia hiyo na katika mabadiliko yanayokwenda kufanyika suala la waandishi wa habari kuwa na viwango vya elimu kwa mujibu wa sheria lizingatiwe.

Aidha Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania Deodatus Balile alifafanua kuwa, suala la sifa na vigezo vya kitaaluma kwa waandishi wa habari limekuwa suala mtambuka na kuulizwa na wadau mbalimbali na wameona ni vyema wakaandaa mjadala maalumu utakaokuwa wazi na wa kitaifa na kila mmoja achangie na kuweza kutoka na makubaliano juu ya sifa kwa waandishi wa habari aidha awe anajua kusoma pekee au awe mtu aliyesomea taaluma hiyo.

Kuhusiana na adhabu kwa kampuni zitakazoshindwa kulipa fedha za matangazo kwa vyombo  Balile ameshauri Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016 na kuwa na kifungu kinachotoa adhabu kwa kampuni  zitakazoshinda kulipa matangazo bila kuwa na sababu za msingi na hiyo itasaidia kupunguza malimbikizo rukuki ya madeni ya matangazo hali inayopelekea vyombo vya habari kushindwa kujiendesha na hatimaye kufungwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...