Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
KAMATI
ya Usalama wilaya ya Kibaha ,imetoa onyo na kupiga marufuku baadhi ya
wafugaji wanaodaiwa kutumia vibaya silaha ya bunduki na kutishia wasio
na hatia ,kwani kwa kufanya hivyo ni uvunjifu wa amani na kinyume Cha
matumizi.
Aidha imerejea
onyo Hilo, kwa matumizi mabaya ya silaha za jadi Kama mishale na upinde
na endapo kutatokea tukio la aina hiyo kamati hiyo haitosita kukomesha
matumizi ya silaha hizo.
Mkuu
wa wilaya ya Kibaha ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Usalama
wilaya,Sara Msafiri alitoa maagizo hayo baada ya kufika Kijiji Cha
Kitomondo ,Kata ya Ruvu Mkoani Pwani na kupata taarifa juu ya baadhi ya
wafugaji wavamizi wanaotishia wakulima na wafugaji wengine kwa silaha
mbalimbali huku wakiingiza mifugo kiholela kutoka ng'ambo.
Alisema
,kibali Cha kumiliki silaha hakiruhusu Raia kutishia Raia mwingine
silaha ,hivyo waaanza kutafakari umiliki wa silaha kwa watu wa aina hiyo
.
"Migogoro yenu malizeni kwa kukaa chini na kuheshimiana,bila ya kutumia bunduki,mishale Wala upinde."
Sara
alisema ,anayachukua majina ya waliohusika na tukio Hilo ili vyombo vya
sheria vikaendelee na uchunguzi na kuchukuliwa hatua ili iwe fundisho
ndani ya jamii.
"Acheni
kuweka sheria mfukoni,achane kudharau vyombo vya sheria, kisa rushwa
,"sitovumilia mambo haya katika wilaya hii,";Natoa Rai na kwa Serikali
za vijiji, maofisa mifugo kufuata na kusimamia Utaratibu wa wafugaji
kuingia katika vijiji ."alisisitiza.
"Kuna
wasiwasi hapa ,Kuna mianya ya rushwa ndio inayotafuna Kijiji
haiwezekani wafugaji wanaingia watakavyo na kuweka sheria mifukoni
wakati wananchi mpo na Serikali ya Kijiji na kata mpo"
Pamoja
na hayo,Sara alikemea mifugo holela na kuagiza Serikali ya kijiji cha
Kitomondo kukutana na wafugaji wiki ijayo ili kubaini wafugaji wavamizi
na idadi ya wafugaji wanaotambuliwa kuomba kibali Halali kwa mkutano wa
Kijiji .
Vilevile mkuu
huyo wa wilaya ,aliielekeza kamati ya usuluhishi ya kijiji na ofisa
mifugo kupitia maboma yote ili kubaini wananchi wanaokodisha wafugaji
ardhi .
Aliwataka
wananchi kuheshimu juhudi za Serikali wakati ikileta Suluhu na kusimamia
changamoto za wakulima na wafugaji wao wanakwenda kuwakumbatia wafugaji
na kuwakodisha ardhi Hali inayosababisha migogoro isiyoisha.
Wakulima
wa Kitomondo ,Kidawa Omary ,Hamza Botea Walisema ,kumezuka wimbi la
mifugo na wafugaji wavamizi Hali inayosababisha kuliwa mazao Yao na
kupata hasara .
Kidawa alisema , mfugaji Dotto Mabula ana maboma mengi ya Mifugo na ndio tishio la wafugaji.
Mfugaji
Michael Mjika alisema ,Chama Cha wafugaji huwa kina kutana na kujadili
changamoto zao ,ambapo amekiri kuwepo kwa wafugaji wavamizi na ambao
wanakiuka taratibu na sheria mbalimbali.
Michael
Lobe ambae amepigwa na baadhi ya watu waliotumwa na mfugaji ambae
amedaiwa kuwa mbabe Dotto Mabula alisema, Juni 9 alivamiwa na kupigwa na
kutishiwa bunduki wakati alipokwenda kumtembelea mkulima mmoja ambae
amemkodisha ardhi kuweka mifugo.
Ofisa
mifugo kata ya Ruvu ,Fransis Ekoni alipokea maagizo hayo na kusema
wafugaji wanaotambulika katika kijiji cha Kitomondo ni wanne tu.
Ombeni
Msangi kaimu mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kibaha,alieleza kuwa,
kuingiza mifugo eneo jingine, Kijiji kingine kwa wakulima ni kosa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...