Mkurugenzi wa Research Publication and Postgraduate Studies (DRPPS), Dkt Eva Luwavi akizungumza na wanafunzi wa cha Taifa  cha usafirishaji (NIT) wakati wa mkutano ulioandaliwa na Chuo hicho na kuongozwa na wahadhiri wa fani mbali mbali kuwaasa na kuwapa ufahamu wanafunzi zaidi 1000 wanaotarajia kuhitimu mafunzo yao chuoni hapo. Mkutano huo umefanyika leo Juni 18, 2022 jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Umahairi wa Kikanda upande wa Usalama Barabarani, Dkt. Omari Mashiakizungumza na wanafunzi wa cha Taifa  cha usafirishaji (NIT) wakati wa mkutano ulioandaliwa na Chuo hicho na kuongozwa na wahadhiri wa fani mbali mbali kuwaasa na kuwapa ufahamu wanafunzi zaidi 1000 wanaotarajia kuhitimu mafunzo yao chuoni hapo. Mkutano huo umefanyika leo Juni 18, 2022 jijini Dar es Salaam.
mlezi wa wanafunzi kutoka Idara ya Ustawi wa Wanafunzi, Meshack Kimaro akizungumza na wanafunzi wenzake, wa cha Taifa  cha usafirishaji (NIT) wakati wa mkutano ulioandaliwa na Chuo hicho na kuongozwa na wahadhiri wa fani mbali mbali kuwaasa na kuwapa ufahamu wanafunzi zaidi 1000 wanaotarajia kuhitimu mafunzo yao chuoni hapo. Mkutano huo umefanyika leo Juni 18, 2022 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wanaotarajia kumaliza masomo yao katika Chuo cha Taifa cha usafirishaji NIT,  wakifuatilia hotuba kutoka kwa  mlezi wa wanafunzi kutoka Idara ya Ustawi wa Wanafunzi, Meshack Kimaro hayupo pichani, akizungumza na wanafunzi wakati wa mkutano ulioandaliwa na Chuo hicho na kuongozwa na wahadhiri wa fani mbali mbali kuwaasa na kuwapa ufahamu wanafunzi zaidi 1000 wanaotarajia kuhitimu mafunzo yao chuoni hapo. Mkutano huo umefanyika leo Juni 18, 2022 jijini Dar es Salaam.

WANAFUNZI zaidi ya 1000 wa chuo cha Taifa cha Usafirisha (NIT) wanaotarajia kumaliza masomo yao wamepewa ufahamu na kuaswa namna ya kwenda kuishi maisha mapya yatakayowasaidia mara baada ya masomo.


Pia wamepatiwa utafahamu wa mambo wanayopaswaa kufanya baada ya kuhitimu ikiwa ni hapa nchini ama hata nje ya nchi.


Wosia huo umetolewa  leo Juni 18, 2022, jijini Dar es Salaam na wahadhiri wa fani mbalimbaliwa wa Chuo hicho wakati wa programu ya kuwaandaa wanafunzi hao kabla ya kumaliza masomo yao.


wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Umahairi wa Kikanda upande wa Usalama Barabarani, Dkt. Omari Mashi akimuwakilisha Makamu Mkuu wa chuo upande wa Taaluma na Ushauri Elekezi.


Akizungumza wakati wa programu hiyo, Dkt Mashi amesema wamewaita vijana hao kwa ajili ya kuwapa ufahamu  kuhusiana na mambo mbali mbali yanayojitokeza mara baada ya kuhitimu masomo yao zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana chuoni na mahali pengine na hata matapeli nyakati zingine wanaotumia fursa za ajira kutekeleza uovu huo 


"Kuna watu wanajifanya waajiri wanakupigia simu na kukueleza juu ya maombi yako ya kazi ukisikia suala la kutoa hela ujue huo ni utapeli". Amesema Mashi


Amesema ni mara ya kwanza kwa Chuo kufanya jambo hili kwani wameona ni muhimu kwa sababu wanapoingia chuoni hapo huwa wanaelekeza jinsi ya kuendeleza maisha yao, Hivyo programu hiyo itawezesha kupata fursa mbalimbali. 


"Waliokuwa na hamu ya kuchukua programu zingine kama master's degree na postgraduate tunawaeleza nini cha kufanya na pia wanaoona wamefikia mwisho wanataka kufanya kazi tunawapa fursa za kazi," ameongeza ma Dkt. Mashi


Licha ya changamoto hizo Dk.Omari ametaka wanazuoni hao kutojiweka nyuma kwenye fursa za kazi pamoja na kujitolea ili kupata uzoefu na ndio maana wahadhili wametumia fursa hiyo kuwapa semina fupi juu ya kuyakabili maisha ya mtaani.


Ameongeza kuwa  wahitimu wa chuo hicho hawakumbani na changamoto ya ajira kwa kuwa chuo hicho kimekuwa na mahusiano mazuri na taasisi na kampuni zenye fursa ya ajira.


Dkt. Mashi alisema chuo chao kina mchango mkubwa katika kuisaidia Serikali katika suala la ajira kwa sababu wanajitaidi kufanya mahusiano au mawasiliano na vyanzo mbalimbali vinavyoweza kuwasaidia wanafunzi kupata ajira.

Ameongeza  kuwa hata walimu wa Chuo hicho pia wamekuwa na mahusiano mazuri na wanafunzi pale inapotokea fursa huwa wanawatafuta kwa njia ya simu na pia hata hapa chuoni wanafunzi wanaofanya vizuri huwa wanabakishwa.


Kwa upande wake, mlezi wa wanafunzi kutoka Idara ya Ustawi wa Wanafunzi, Meshack Kimaro amewasihi wanafunzi hao wakaishi kwa wema kwenye jamii.


"Mkaendeleze mema mkawe raia wema mtakaoheshimika mkaishi kama watu mlioelimika watu wenye maadili mema mkazingatie kuwa maisha yanaendelea"amesema.


Amewataka wahitimu hao wakaitumie elimu yao kwenye ujenzi wa Taifa  "mkahikikishe mnayasimamia malengo yenu na mhakikishe mnalijenga taifa"


Naye, Mkurugenzi wa Research Publication and Postgraduate Studies (DRPPS), Dkt Eva Luwavi amewaambia wanafunzi hao kuwa elimu waliyoipata bado ni ndogo wanatakiwa waendelee kusoma.


"Lazima muongeze elimu hii haitoshi maisha yamebadilika sio kama zamani, zamani wazazi wetu walikuwa wanaoona ukipata shahada ya kwanza ndiyo umemaliza lakini kwa sasa haitoshi, "amesema Dkt. Luwavi.

Aidha amewasihi wanafunzi wasiache kujiendeleza kielimu baada ya kumaliza elimu zao.

Amewapa mbinu za kusoma ni pamoja na kuwania kusoma Postgraduate Diploma mara baada ya kumaliza masoma yao.


Naye, Neema Vicent mhitimu wa chuo hicho ameeleza kuwa Wahadhiri wa chuo hicho wameaandalia mafunzo mafupi yaliyolenga kuwapa mwanga katika maisha ya nje ya chuo.


Japhet Makame mhitiwa wa chuo hicho amesema kuwa elimu tuliyopewa imetuandaa kuyakabili maisha ya mtaani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...