…TUNAKOKWENDA KUNA KILA KITU
Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
WAKAZI wa Taarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha ambao wameamua kuhama kwa hiyari
yao kwenye eneo la hifadhi wamesema wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa
upendo mkubwa aliouonesha kwao kwa kuhakikisha nao wanakuwa na makazi ya kudumu
eneo la Msomela wilayani Handeni mkoani Tanga
Wakizungumza huku wakiwa wanaezua nyumba zao wenywe tayari kwa kuhama wakazi kwa hiyari wamesema walikuwa wanaisubiri fursa hiyo kwa
muda mrefu lakini Rais Samia ameitekeleza, hivyo wanamshukuru sana kwa uamuzi
wake.
Mkazi wa Kijiji cha Kimba wilayani Ngorongoro Beatrice Soka amesema amefurahi sana kwasababu kwa
muda mrefu walitamani mchakato huo ufanyike lakini ulichelewa.“Kwa hiyo tamko
hili lilipoletwa kwa kweli mimi ni miongoni mwa watu tuliojiandikisha kwa
hiyari yangu pamoja na familia yangu kwa ajili ya kwenda huko Msomela.
“Bahati nzuri nimekwenda huko Msomela na nimerudi jana.Nimeshuhudia mwenyewe kwa
macho yangu na akili zangu kwa kweli fursa tuliyopewa na Rais Samia ni ya
kipekee, ni ajabu, ni fursa ya upendeleo kwa wana Ngorongoro wote.
“Kuna shule, huduma ya maji , miundombinu yote na kuna mabwawa ya kutosha,
nyumba, mzunguko wa nyumba kuna ekari tatu mbali na mashamba yalipo nje ya pale
ekari tano na mama Samia ametuwezesha tuliotoka hapa tuweze kwenda kuendelea na
kasi kwani tumepoteza muda.
Kwa upande wake Pasihaya Parakoi Seseka ambaye ni miongoni mwa wakazi wa Tarafa
ya Ngorongoro ambaye amuamua kuhama kwa hiyari yake
Akizungumza baada ya kushuhudia zoezi hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe John Mongela amesema zoezi hilo ni la hiyari na waliyoamua kuondoka wamefikia hatua hiyo baada ya kujadilina na familia zao na kuafiki mpango huo bila kulazimishwa.
Mmoja wa Wafanyabiashara,aliekuwa akimiliki eneo la kupumzikia Wageni (guest house) katika kijiji cha Kimba, Ngongoro Samwel Danniel Huho akianza kuezua paa la nyumba yake akiwa ni miongoni mwa Wananchi wa kijiji hicho waliomua kuondoka kwa hiari ili kuhama eneo hilo kupisha Uhifadhi ndani ya Ngorongoro na kuhamia katika kijiji cha Msomela, Kata ya Misima, wilayani Handeni, ambako ni makazi mapya ya wananchi wanaohamia kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro mkoani Arusha.

MKazi wa kijiji cha Kimba tarafa ya Ngorongoro ndani ya eneo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro katika mkoa wa Arusha, Pasihaya Parakoi Seseka akiezua paa la nyumba yake akiwa ni miongoni mwa Wananchi wa kijiji hicho waliomua kuondoka kwa hiari kwenda kwenye kijiji cha msomela wilayani Handeni ikiwa hatua ya awali ya utekelezaji wa makubakino ya kupisha uhifadhi endelevu katika eneo hilo la urithi wa Dunia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...