Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

NAOMBA nianze kwa kusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, nawe nijibu Kazi Iendelee. Ndio lazima kazi iendelee na wote tunaowajibu wa kujenga Taifa letu la Tanzania

Taifa la Tanzania tulivu, Tanzania yenye amani,Tanzania yenye Umoja na mshikamano, Kazi iendelee kwenye Taifa ambalo sasa liko kwenye mikono salama ya Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Ni Rais Samia nchi yetu inakwenda salama salmini.

Baada ya utangulizi wa salamu naomba nieleze wazi na mapema, nimevutiwa na siasa zinazofanywa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Shaka Hamdu Shaka.Kwa Shaka nimekuwa sina shaka na harakati anazofanya katika medani za kisiasa na hasa katika kuwatumikia Watanzania kupitia Chama chake.

Shaka ni miongoni kwa wanasiasa vijana wa Chama hicho ambao wamepata nafasi ya kupewa nafasi kubwa za uongozi.Yaani Shaka ndio msemaji wa CCM ,nimetumia lugha rahisi nieleweke maana nikisema Katibu wa Itikadi na Uenezi huenda wengine wasinielewe.

Ninaposema navutiwa na siasa na Shaka Kuna sababu nyingi, miongoni mwa sababu ni pamoja na uwezo wake wa kujenga hoja hasa zinazohusu maslahi mapana ya Watanzania.Shaka anajua kupigania maslahi ya walio wengi.

Ndio namzungumzia Shaka ambaye kwenye safari yake ya kisiasa amepita kwenye mabonde na milima . Pamoja na milima mikali katika safari yake ya kisiasa amebaki kuwa bora,amebakia kuwa kijana wa mfano.

Shaka hana makuu, uzungumzaji wake katika kutetea maslahi ya walio wengi yanaonekana usoni,machoni na moyoni . Shaka Hamdu Shaka amejaaliwa kuwa na sauti yenye Mamlaka, akisema wanasikia, akitoa maelekezo yanatekelezwa . Kwangu namuona Shaka ni moja ya wanasiasa vijana ambao huko mbele ya safari wanaweza kuwa mbali katika medani za kiongozi.

Tuachane na hayo, nisije nikaambiwa namsifia sana lakini ukweli unabaki pale pale anayestahili sifa apewe sifa yake Shaka kwa kazi anayofanya ndani ya Chama chake anastahili sifa , anastahili kupewa heshima yake, anastahili kutambuliwa kwa thamani ya nyota tano.

Kwanini Shaka anastahili sifa, nataka nikueleze nimekuwa nikifuatilia ziara zake ambazo anazifanya kwenye mikoa mbalimbali nchini.Siku za karibuni alifanya ziara katika Mkoa wa Manyara, moja ya mambo aliyoyafanya akiwa mkoani Manyara ni kujitambulisha kwa WanaCCM.

Shaka mbali ya kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi , Chama chake kimempa jukumu la kuwa Mlezi wa Mkoa huo nafasi ambayo awali alikuwa nayo Mzee Mizengo Peter Pinda, ni Pinda ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Taifa hili wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya mzee wa Msoga Jakaya Kikwete.

Lakini Shaka alipokuwa Manyara alifanya kazi kubwa mbili, moja ya kukagua Uhai wa Chama kwa kuzungumza na wanachama wa Chama hicho kwenye ngazi ya mashina pamoja na mikutano ya ndani ambayo viongozi wa Chama na Serikali waliitumia kutoa taarifa za utekelezaji wa Ilani na hali ya kisiasa.

Kazi ya pili iliyofanywa na Shaka ilikuwa ni kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita imetoa fedha nyingi kuhakikisha inatekelezwa na sio kutekelezwa tu bali ni kwa wakati na thamani ya fedha iendane na ubora.

Shaka hakusita kutoa maelekezo pale alipoona Kuna mambo hayako sawa. Cha kufurahishwa Serikali haikuwa nyuma, kila Shaka alikokwenda viongozi wa Serikali na Chama walikuwepo. Hakika nilijifunza jambo kwa Shaka nalo ni ufuatiliaji wa kila jambo.

Ziara ya Manyara ikawa ya mafanikio makubwa na akiwa katika Mkoa huo alitoa maelekezo kwa wateuliwa Rais wakiwemo wakuu ws Wilaya, mikoa na wakurugenzi kujenga tabia ya kuelezea yanayofanywa na Serikali kwenye maeneo yao .

Katika hilo akatoa angalizo kwamba anayo mashaka kwa baadhi ya wateule kwanini wamekuwa kimya, kwanini hawasemi yanayofanyika wakati kwenye Serikali ya Awamu ya Tano walikuwa wakijitokeza ba kuelezea mafanikio. Kwa Mama Samia wako kimya, Kuna nini?Jibu la ukimya wa wateule wanalo wenyewe, nawaachia wenyewe.

Baada ya ziara ya Manyara, Shaka akarejea Dodoma na kisha akaungana na Rais Samia mkoani Tabora ambako kulikuwa na uzinduzi wa barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami, Shaka baada ya Tabora ,akaamua kufanya ziara katika Mikoa ya Lindi na Mtwara, amefanya kazi kubwa na nzuri kwenye mikoa hiyo.Kazi aliyoifanya mikoa ya Kusini ni kubwa.

Nikiri ziara ya mikoa ya Kusini imekuwa yenye mafanikio makubwa tena makubwa kweli kweli. Akiwa katika Mikoa hiyo mbali ya kuzungumza na wana CCM alipata nafasi pia ya kuzungumza na Wananchi, alitoa nafasi ya kusikiliza matatizo yanayowakabili Wananchi kwenye maeneo husika, amepokea malalamiko mengi.

Nakumbuka akiwa mkoani Lindi mbali ya Wananchi kutoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwaletea maendeleo, pia alipokea na changamoto,kwa mfano Wananchi hawakusita kuelezea uharibifu unafanywa na wanyama pori hasa tembo ambao wamevamia mashamba na kuharibu mazao, pamoja na makazi ya Watu .

Katika hilo Shaka alitoa maelekezo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia njia sahihi ya kuondoa tembo wavamizi .Mbali ya tembo wanchi wakatoa kilio cha kuchelewa kwa pembejeo za kilimo hasa kwa wakulima wa korosho .

Shaka akaonesha shaka kwa nini pembejeo zimechelewa wakati Rais Samia alishazitoa kwa ajili ya wakulima, pembejeo ambazo zimetolewa bure na Serikali.Hapo akatoa maelekezo kwa viongozi wa mikoa hiyo.

Changamoto nyingine Shaka ambayo alielezwa na Wananchi hasa wa Tandahimba mkoani Mtwara ilikuwa ni ya upatikanaji wa maji safi na salama. Katika hilo Shaka akaona isiwe tabu akafanya mawasiliano na Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa njia ya simu.

Mawasiliano ambayo yameacha tumaini jipya kwa wananchi baada ya kupata taarifa Kuna mkakati kabambe wa Serikali wa kuondoa changamoto ya maji.Wananchi wakabaki wanapiga makofi ya furaha, Chama kimefika na ufumbuzi unapatikana.

Kuhusu changamoto ya miundombinu ya barabara nayo ilikuwa kilio kikubwa kwa wananchi wa Tandahimba na Newala lakini nayo majibu yake yalikuwa mazuri.Shaka alifanya mawasiliano na viongozi wa Serikali na majibu yakawa tayari Rais Samia ameshapata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo imebeba uchumi wa Kusini .

Ni Shaka ambaye akiwa kwenye ziara yake amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kukwama kwa miradi ya maendeleo kutokana na sababu mbalimbali ambazo nyingine zinatokana na uzembe wa baadhi ya watendaji wa Halmashauri na hakusita kutoa maelekezo.

Kilichokuwa kinafurahisha zaidi Shaka kwenye ziara ya mikoa ya Kusini aliamua kutoa nafasi kwa wananchi kupata muda wa kutosha kuuliza maswali kuhusu miradi ya maendeleo.

Katika hilo wapo watumishi wa Umma hasa wakuu wa Idara walikuwa kwenye wakati mgumu, wanatoa maelezo lakini Wananchi wanakataa.Hivyo Shaka aliwabana watendaji wa Serikali hadi walipokuwa wanatoa majibu ambayo Wananchi waliridhika nayo.

Hakuwa tayari kuwa upande wa Serikali, alisimama na Wananchi alihakikisha maswali yote ambayo Wananchi wanauliza wanapata majibu tena majibu ya uhakika.Viongozi wa Serikali ngazi ya Wilaya na mikoa hawakuwa na namna ya kukwepa Shaka aliwahakikishia yote ambayo yameelezwa kama changamoto yatapatiwa ufumbuzi.

Katika baadhi ya mambo ambayo Shaka alionesha kuwa na Mashaka nayo hakusita kuwaambia viongozi wa Serikali kuwa hataki kuwa mbuzi wa kafara,wenye Mamlaka lazima wawajibike kwa kutatua migogoro ambayo mingine ni ya muda mrefu na Serikali ilishatoa maelekezo.

Kwa mfano moja ya mgogoro ambao Shaka ametaka upatiwe ufumbuzi ni Ile unaohusu mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege.Katika mgogoro huo mbali ya kukataa kuwa mbuzi wa kafara ametoa maelekezo kwa wahusika.

Hakika Shaka katika ziara hiyo alisimama upande wa wananchi kwa asilimia 100.Lakini hakusita kuwahakikishia yale yote ambayo ameyaona atayafakisha kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pamoja na yote nikiri nilifurahishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye wakati wa kikao Cha majumuisho ya ziara ya Shaka katika Mkoa wa Lindi aliamua kushiriki.

Alishiriki majumuisho hayo na akatoa maelekezo kwa watumishi wa umma kuhakikisha yote ambayo yametolewa maelekezo na Shaka kwa niaba ya CCM yanatekelezwa.Waziri Mkuu hakusita kuelezea kila jambo ambalo linahitaji ufumbuzi Serikali itachukua hatua.

Naomba nihitimishe kwa kusema hivi Wana CCM msiwe na shaka kwa Shaka.Kubwa zaidi la kufurahishwa ni mafaniko makubwa yaliyopatikana kwenye ziara yake ya mikoa ya Kusini.Wakuu wa mikoa hiyo kila mmoja Anaendelea kutekeleza yaliyotolewa maelekezo na CCM kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi

INATOSHA kwa leo.

0713833822













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...