Kikundi cha Wanawake wa Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga (UMS) wamemuomba Waziri Dkt. Doto Biteko awape leseni ya Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika kijiji cha Nyamishiga Kata ya Lunguya.

Wamesema kuwa serikali imewakabidhi Rush ambazo mpaka sasa wanazisimamia vyema na wanakusanya maduhuli ya serikali na kuongeza kuwa iwapo watapata leseni watafanya vizuri zaidi.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Levina Onesmo aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa Michuzi Blog katika eneo la machimbo ambapo alisisitiza ombi lao lifanyiwe kazi haraka kwa kuwa RUSH ni ya muda mfupi kwa mujibu wa taratibu za tume ya madini ukilinganisha kwa sasa wanawake wamekuwa wajasili na wanahitaji kunufaika.

Wanawake hao wameiomba Wizara na tume ya Madini kuendelea kuwaamini wanawake kwenye sekta hiyo kwani ni waaminifu huku akitolea mfano kuwa mwanawake ni nidereva mzuri na ni nadra sana kupata ajari mbaya wakati akiendesha gari barabarani, anakuwa ni mwangalifu na kwamba serikali itumie uaminifu huo kuwapa leseni.

 Emmanuel Charles ni mmoja kati ya viongozi kwenye eneo la mgodi amekili kuwa Wanawake ni waaminifu, hivyo ameunga mkono serikali iwaamini na kendelea kuwapa fursa ya kusimamia maeneo yanayoibukia kuwa na Madini ya Dhahabu.



 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...