KATIKA kuhakikisha mtoto wa jinsia ya kike anapata Elimu bora sawa na mtoto wa jinsia ya kiume, Jamii imeaswa kuachana na dhana potofu ya kuwabagua watoto wa kike katika upatikanaji wa Elimu hiyo.

Akizungumza katika Mkutano wa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa Nguzo Nane Wilayani Maswa, Mkoani Simiyu, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ndugu Daniel Chongolo amewaasa Wazazi wa watoto mkoani humo kuhakikisha watoto wa kike wanapata haki yao ya msingi ya kwenda Shule sawa na watoto wa kiume.

“Acheni dhana ya kuwalazimisha watoto wa kike waolewe ili Wazazi mpate Ng’ombe, watoto wa kike sio mtaji wa ninyi kupata Ng’ombe, na wao wanastahili kusoma kama wenzao wa kiume”, amesema Chongolo.

Amesema kuwa endapo watoto hao wa kike watakwama kwenda Shule watashindwa kufanya maamuzi na kutafakari kwa kina sanjari na kuleta tija kwenye Jamii zinazowazunguka.

Chongolo ametoa wito kwa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya hiyo na Uongozi kusimamia kikamilifu na kuhakikisha watoto wa kike katika Mkoa huo wa Simiyu wanapata haki zao za msingi ikiwa pamoja na kupelekwa Shule kwa ajili ya kupata Elimu bora.

“Elimu ni urithi kwa Mtoto yeyote yule, na mtoto wa kike anastahili kupata urithi huo kama mtoto wa kiume , hata hivyo sisi Vijana wa kiume wa sasa hivi tunataka Wake waliosoma vizuri ili tusaidiane katika kupambana na maisha na kutokomeza umaskini”, ameeleza .

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...