WATUMISHI wa sekta ya afya walio katika mafunzo ya Epidemiolijia kwenye mikoa ya Shinyanga na Tabora wamepongeza Chuo Kikuu Mzumbe kupitia mradi wa ‘CDC’ kwa kufadhili mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya yaliyolenga kuwajengea uwezo katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko,kufanya tafiti na uchakataji wa taarifa za afya.
Akizungumza na Timu ya ufuatiliaji wa mafunzo hayo wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga, Dkt.Raymond Tibakya ambaye ni Mganga katika hospitali ya Wilaya ya Kishapu ya Dkt.Jakaya Kikwete, amesema mafunzo hayo yamemsaidia kufahamu kwa undani kuhusu mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa, hatua iliyomwezesha kufanya uchunguzi kuhusu mfumo wa ufuatiliaji wa afya kwa Wakinamama wanaoishi na Virusi vya UKIMWI,kubaini mapungufu na kutoa mapendekezo kuhusu mfumo huo pamoja na kufanya utafiti kuhusu ongezeko la Virusi vya UKIMWI katika damu kwa Wagonjwa wanaoendelea na matumizi ya dawa za kufubaza virusi.
Aidha Dkt Tibyaka ameongeza kuwa kupitia mafunzo hayo aliweza kujumuika kwenye timu iliyoundwa kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu uliotokea katika wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma na kufanikiwa kuutokomeza kupitia ujuzi alioupata katika mafunzo hayo na kushukuru wafadhili wa Mradi huo Serikali ya Marekani kupitia PEPFAR na Kituo cha kudhibiti na kujikinga na maradhi DCD kupitia mradi unaotelekezwa na Chuo Kikuu Mzumbe.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mkoani Tabora Watumishi wa Hospitali Teule ya wilaya ya Sikonge Dkt.Neema Wilson na Bw. Laurent Lushekya, ambaye ni Afisa Afya wa wilaya hiyo wamewapongeza waratibu na kusema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwani hadi sasa yamewasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi tofauti na hapo awali na kuahidi kuutumia ujuzi huo kutatua changamoto za afya wilayani humo ambapo pia wameshukuru kuwezeshwa kupata mafunzo hayo.
Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi na Mratibu wa mafunzo hayo katika mradi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Dkt.Laurencia Mushi, amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuisaidia Serikali kuimarisha mifumo ya afya nchini kwa kuwaongezea ujuzi Watumishi wa afya kupitia vyuo vya Umma na kuongeza kuwa, hadi sasa Watumishi 15 wamehitimu mafunzo hayo katika awamu ya kwanza na 15 wengine wanaendelea na mafunzo na kwamba program hiyo ni ya miaka mitano kuanzia mwaka 2021 hadi2025.
Timu ya ufuatiliaji baada ya mazungumzo na Mkuu wa mkoa wa Tabora
Timu ya ufuatiliaji wakiwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Timu ya ufuatiliaji ya Wizara ya Afya na Chuo Kikuu Mzumbe wakisaini kitabu cha Wageni walipowasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Shinyanga.
Wanafunzi wa mafunzo ya Epidemiolojia wa wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wakiendelea na mafunzo kwa vitendo.
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoani Tabora Bw.Selemani Ally akizungumzia mafanikioyaliyopatikana katika sekta ya afya wilaya yake kutokana na Watumishi wake kupokea mafunzo hayombele ya timu ya ufuatiliaji.
Wanafunzi wa mafunzo ya Epidemiolojia wa wilaya ya Sikonge mkoani Tabora Dkt.Neema Wilson (kulia) na Afisa Afya Bw.Laurent Lushekya (katikati) wakipokea mafunzo kwa vitendo kutoka kwa
Mkufunzi Msaidizi Bw.Pius Tarimo.
Timu ya ufuatiliaji wa mafunzo wakizungumza na bi.Celina Mpemba (katikti) ambaye ni Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Shinyanga akitoa maoni yake kuhusu mabadiliko chanya yaWafanyakazi wenzake waliopokea mafunzo hayo. Kulia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbena mratibu wa mafunzo hayo kupitia mradi wa CDC Dkt.Laurencia Mushi,kushoto ni bi Nsiande LemaMshauri Mkazi wa mafunzo ya Epidemiolojia ngazi ya awali kutoka Wizara ya Afya.
Mwanafunzi wa mafunzo ya Epidemiolojia Bw.Laurent Lushekya na Mhadhiri Mwandamizi wa ChuoKikuu Mzumbe Dkt.Laurencia Mushi wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Sikonge katikakikao cha utambulisho.
Picha na Emmanuel Massaka, Michuzi Tv


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...