Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

WAZIRI wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amesema kuwa adha ya ukosefu wa rasilimali Maji katika mkoa wa Dar es Salaam ilimnyima usingizi huku akitoa wito kwa Wasimamizi na Wataalamu wa rasilimali hiyo kuwa makini na Maji hayo ambayo yanaweza kupotea muda wowote.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Tano wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika Usimamizi na Maendeleo ya Rasilimali Maji, Waziri Aweso amesema katika nafasi yake ya uongozi, akiwa Waziri wa Maji hatosahau adha hiyo iliyowakumba Wananchi wa Dar kwa ukosefu wa Maji sehemu kubwa ya mkoa huo.

"Adha ya Maji, Dar es Salaam iwe funzo kwetu Wasimamizi wa Rasiliamli Maji, na tujue kuwa Maji tunayoyaona kila siku, kila kukicha lakini yanaweza kutoweka muda wowote", amesema Waziri Aweso.

Aidha, Waziri Aweso amesema atakuwa kinara kuhakikisha anawabana Wataalamu wa Maji na kuhakikisha ushirikiano baina ya Viongozi wa Sekta hiyo ya Maji wanatoa elimu na kuwashirikisha wadau wengine waliokuwa katika Sekta mtambuka.

"Maafisa wa Mabonde ya Maji yote, hamuwezi kufanya kila kitu peke yenu, hakikisheni mnashirikisha Jamii katika masuala ya kulinda vyanzo vya Maji, naamini ukishirikisha Jamii utafanikiwa lakini usiposhirikisha Jamii hiyo utakwama, kwa sababu Jamii ipo kila siku", ameeleza Waziri Aweso.

Hata hivyo, baada ya kusomwa Bajeti Kuu ya Serikali, Waziri Aweso amesema ataanza ziara kwenye Mabonde yote Tisa nchini, ili kutoa elimu kwa Wananchi wa waliopo karibu na maeneo hayo ili kuhakikisha utunzaji bora wa vyanzo vya Rasiliamali Maji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali Maji kutoka Wizara ya Maji, Dkt. George Lugomela amesema Jamii ina wajibu wa kupanga matumizi ya Maji katika shughuli za mbalimbali za kiuchumi, na kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kukua kwa kasi.

Naye, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika Usimamizi na Maendeleo ya Rasilimali Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba amesema tafiti mbalimbali zimefanyika ili kujua thamani ya Rasiliamali Maji na kuipa thamani kama Sekta nyingine zinavyopewa thamani.

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akizungumza na Wadau wa Mkutano wa Tano wa Jukwaa la Kitaifa la Sekta Mtambuka katika Usimamizi na Maendeleo ya Rasilimali Maji, mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika Usimamizi na Maendeleo ya Rasilimali Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba akizungumza katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Sekta mbalimbali waliohudhuria mkutano wa tano wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika Usimamizi na Maendeleo ya Rasilimali Maji, mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Rasilimali Maji kutoka Wizara ya Maji, Dkt. George Lugomela akizungumza katika mkutano huo.

 Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (wa tatu kutoka kulia) akionyesha Ripoti ya Mpango Mkakati wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika Usimamizi na Maendeleo ya Rasilimali Maji, ripoti imezinduliwa kwenye mkutano huo kwa ajili ya utekelezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...