BAADA ya kutokea sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii hapo jana kuhusu kupanda kwa gharama ya bei ya umeme, Waziri aliyepewa dhamana ya kusimamia Wizara ya Nishati, Mh. January Makamba, ametatua utata huo hivi leo tarehe 9 Juni Bungeni jijini Dodoma.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nyasa kupitia tiketi ya CCM, Mh. Stella Manyanya aliyeuliza kuhusu uvumi huo kwenye mitandao ya kijamii. Mh,January Makamba amekanusha uvumi huo kwa kujibu kwamba, “Si kweli kwamba bei ya umeme imepanda, na Serikali inasikitishwa sana na kuvumishwa kwa taarifa hiyo ya uwongo”.

Mh. January Makamba mbele ya Bunge tukufu amesema kwamba, ameshaziomba mamlaka husika kuchukua hatua stahiki kwa wale wote wanaovumisha taarifa hiyo ya uzushi kuhusu kupanda kwa bei ya umeme nchini.

Mh January pia alitoa ufafanuzi ya kwamba, mchakato wa kupanda au kushuka kwa bei ya umeme si mchakato wa siku moja na wala haufanywi kwa siri, bali mchakato huu huusisha maombi ya TANESCO kwa EWURA na pia ni lazima Wananchi wahusishwe ili kutoa maoni yao ili mchakato ukamilike.

Hivyo basi, taarifa ya kwamba bei ya umeme imepanda, si ya kweli na ipuuzwe, amesema Waziri January Makamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...