
Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Tanzania ya Wanawake ya Kriketi kwa kufanya vizuri na kuongoza kwenye mashindano ya Kwibuka Cup yanayoendelea nchini hivi sasa nchini Rwanda.
Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo leo Juni 15, 2022 alipoongea na simu timu hiyo kupitia kwa Nahodha wa timu hiyo .
Amesema anaipongeza timu hiyo baada ya kuzishinda timu zote walizokutana nazo kwenye mashindano hayo na kuwa kinalani mwa mashindano hayo.
Amezitaja timu hizo kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana na Ujerumani bado timu ya Nigeria na Brazil ambapo wakishinda mechi mojawapo wanaingia fainali za mashindano hayo.
Aidha, amemshukuru Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo kwa kuwa karibu na timu hiyo katika kipindi chote huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuisaidia timu hiyo ili ifike mbali zaidi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...