
Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) Sarah Gordon-Gibson akizungumza jambo wakati wa tukio la ukabidhiwaji wa msaada wa unga wa mahindi tani 12000 ambazo zimetolewa na Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo(USAID) kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wanaoishi kwenye kambi mbili za wakimbizi zilizopo mkoani Kigoma.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk.Donald Wright akichota unga wa mahindi kwenye bakuli na kuweka katika sufuria wakati alipokuwa anapika ugali ikiwa ni ishara ya kukabidhi chakula kwa wakimbizi wanaoishi kwenye kambi mbili zilizopo mkoani Kigoma.Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani Sudi Mwakipesi(katikati) na Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) Sarah Gordon-Gibson
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani Sudi Mwakipesi akitoa akizungumza wakati wa tukio hilo la Marekani wakikabidhi msaada wa unga wa mahindi kwa WFP ili kupelekewa wakimbizi wanaoishi katika kambi zilizipo mkoani Kigoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani Sudi Mwakipesi(katikati) akisonga ugali wakati wa tukio la kukabidhiwa kwa unga wa mahindi tani 12000 ambazo zimetolewa na Marekani na kukabidhi kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP).Wengine kwenye picha hiyo ni Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk.Donald Wright(kulia) na Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) Sarah Gordon-Gibson(kushoto).
Ugali ukiwa mezani baada ya kuiva
Sehemu ya shehena ya unga wa mahindi ambayo yametolewa na Marekani na kisha kukabidhi kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) .Msaada huo wa unga ni kwa ajili ya wakimbizi wanaoishi kwenye kambi mbili za wakimbizi zilizopo mkoani Kigoma.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk.Donald Wright akielezea hatua ambazo nchi yake inachukua katika kusaidia katika kutoa huduma mbalimbali ikiwemo msaada wa chakula kwa ajili ya wakimbizi wanaoishi katika kambi za wakimbizi zilizopo mkoani Kigoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...