Raisa Said,Korogwe


HALMASHAURI ya Wilaya ya Korogwe imesema itawachukulia hatua baadhi ya
wazazi wanaowaachisha watoto wao masomo na kuwapeleka kufanya kazi za
ndani mijini.

Onyo hilo limetolewa na Afisa Maendleo ya Jamii kaika Halmashauri ya
Wilaya ya Korogwe David Mpumiwa kwenye sherehe za kuadhimisha Siku ya
Mtoto wa Afrika iliyofanyika ngazi za Wilaya katika Kijiji cha Lusanga
katika kata ya Mnyuzi wilayani Korogwe.

Mpumilwa, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya (DED),
alisema kuwa kuwaachisha watoto, hasa wasichana masomo na kuwapeleka
katika kazi za ndani ni unyanyasaji na kuwanyimwa haki ya watoto
kufuata na kufikia ndoto zao za ma isha na kinyume cha sheria.

Mpumilwa ingawa hakutaja idadi ya watoto wa aina hiyo ambao
wameachishwa masomo akasema baadhi ya kesi hizo sasa zinashughulikiwa
na Jeshi la Polisi. Alisema tu kwamba baadhi ya wazazi walikuwa bado
wanaendelea kudumisha tabia hiyo katika eneo hilo.

Alisema inasikitisha kuona tatizo hilo likiendelea katika kata zenye
Kamati za Mpango wa Taifa kwa ajili ya kutokomeza Ukatili dhidi ya
Wanawake na Watoto (MTAKUWA).

"Tunawapa wazazi ambao wamesaidia watoto wao kutoroka shuleni kuripoti
kwa Maafisa Watendaji wa kata siku ya Jumatatu wakiwa na watoto wao au
ama sivyo watachukuliwa hatua za kisheria,” Mpumilwa aliamuru.

Mpumilwa alikemea tabia ya kuwatumia watoto chanzo cha kuwaingizia
kipato akisema ajira ya watoto haikubaliki katika aina zake zote.

Mpumilwa aliipongeza shirika la World Vision Tanzania (WVT) kwa kuendeleza
programu zinazojihusisha na kuimarisha ulinzi wa watoto ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa miundombini ya afya, elimu na maji.

Ofisa Ustawi wa Jamii katika halmashauri hiyo, Richard Nchimbi alitoa
wito jamii kubadilika, akisema kuwa ni aibu kuona mimba za utotoni,
utoro ukiendelea pamoja na uwekezaji wote ikifanywa na shirika la
World Visiona katika Kata hiyo.

Aidha alikemea tabia ya wazazi kusuluhisha masuala ya unyanyasaji wa
watoto nyumbani na kuzuia serikali kuwadhibu wahalifu.

Awali Mratibu wa World Vision WVT mradi wa Mnyuzi ADP, Samuel Charles, alisema kuwa shirika limechukua hatua ya kuanzisha na kuimarisha kamati za
MTAKUWA katika vijiji 12 katika kata mbili za Mnyuzi na Kwagunda

Pia wameimarisha na kuanzisha Mabaraza ya watoto katika shule za
msingi kwa kushirikiana na serikali ili kuwawezesha watoto kupaza
sauti zao dhidi ya unyanyasaji ambao unajulikana kutendwa zaidi na
ndugu na jamaa wa karibu wa watoto hao.

Aidha amesema kwenye jamii bado yapo matendo kama ndoa za utotoni,kulazimishwa,mimba za utotoni,ukeketaji na vipigo katika familia hivyo serikali inatakiwa kwa kushirikiana na wadau kupingana na mambo hayo.

Hata hivyo katika maadhimisho hayo shirika hilo la World Vision Tanzania kupitia eneo la Mnyuzi waliweza kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo madaftari na mabegi ya shule Kwa watoto waliofanya vizuri katika mitihani ya darasa la nne .

Mratibu wa World Vision mradi wa Mnyuzi ADP, Samuel Charles  akimkabidhi zawadi  ya begi  mmoja wa wanafunzi  aliyefanya vizuri  katika mtihani wa darasa la nne Wilayani korogwe mkono Tanga

Mratibu wa World Vision (WVT) mradi wa Mnyuzi ADP Samuel Charles



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...