Na Janeth Raphael
Dodoma Ina wakazi takribani 500,000 na kati ya hao asilimia 82 wanapata huduma ya  maji safi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Dodoma ( DUWASA) Mhandisi Aron Joseph ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma.

Mhandisi Aron amesema mahitaji ya maji katika jiji hilo ni lita milioni 133 Kwa siku ( MWAKA 2022) na yataongezeka hadi kufikia lita  milioni 204 kwa siku kufikia mwaka 2036 na uwezo wa kuzalisha maji ni lita milioni 67.1 Kwa siku.

Aida Mhandisi huyo amebainisha kuwa DUWASA kwa kushirikiana na Wizara ya maji imeendelea na utafiti wa namna bora ya kuendelea na kasi ya mahitaji kwa kubuni mbinu mbalimbali za utatuzi wa changamoto ya uhaba wa maji safi na uondoshaji maji maji taka kwa kuanzisha utekelezaji wa mipango ya dharura, muda mfupi, kati na mrefu ili kuongeza kiasi cha upatikanaji wa maji katika jiji hilo.

Mhandisi Aron amewakumbusha wakazi wa Dodoma kutunza miundombinu ya maji safi na maji taka na kutunza vyanzo vya maji kwa kuboresha Mazingira hasa Kwa kupanda miti na utunzaji wa miti hiyo.

" Tunzeni miundombinu ya maji safi na maji taka, matumizi sahihi ya maji na kuhifadhi maji, matumizi sahihi ya mtandao wa maji taka na kulipa akara za maji kwa wakati" - Mhandisi Aron Joseph.

Wakati huo huo Mhandisi Aron amewakumbusha wananchi juu ya swala la sensa linalotarajiwa kufanyika mwezi wa nane mwaka huu 2022.

"Mbele yetu tuna zoezi la sensa ya watu na makazi nitumie fursa hii kuwaomba wananchi wote kujitokeza kwa wingi ili kuhesabiwa ifikapo tarehe 23 mwezi wa nane mwaka huu, sensa ya watu na makazi ni muhimu sana Kwa ustawi wa Taifa letu" - Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Aron Joseph.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...