Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Ruvuma, Bakari Ally Mketo akikata utepe kuzindua moja ya matrekta yanayotolewa na benki ya Benki ya Taifa ya Biashara ya NBC kwa wakulima.Mkopo huo ambao ni sehemu ya huduma ya NBC Shambani, unatolewa kwa masharti nafuu ambapo mteja atalipa asilimia 25 kama malipo ya awali na kiasi kilichobaki kulipwa kwa awamu kuanzia mwaka mmoja hadi mitano.Kulia ni Meneja wa Tawi la NBC Songea, Frank KirangaKatibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Ruvuma, Bakari Ally Mketo akikabidhi treka kwa mkulima, Chacha Marwa Mwikwabe baada ya kufanikiwa kuwa mteja wa kwanza kupata mkopo kutoka Benki ya Biashara ya Taifa NBC.Mkopo huo ni sehemu ya huduma ya NBC Shambani, inatolewa kwa masharti nafuu ambapo mteja atalipa asilimia 25 kama malipo ya awali na kiasi kilichobaki kulipwa kwa awamu kuanzia mwaka mmoja hadi mitano.Kulia ni Meneja wa Tawi la NBC Songea, Frank Kiranga Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Ruvuma, Bakari Ally Mketo akikata utepe kuzindua moja ya matrekta yanayotolewa na benki ya Benki ya Taifa ya Biashara ya NBC kwa wakulima.Mkopo huo ambao ni sehemu ya huduma ya NBC Shambani, unatolewa kwa masharti nafuu ambapo mteja atalipa asilimia 25 kama malipo ya awali na kiasi kilichobaki kulipwa kwa awamu kuanzia mwaka mmoja hadi mitano.Kulia ni Meneja wa Tawi la NBC Songea, Frank Kiranga.

  Ruvuma. Julai Mosi, 2022.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua rasmi huduma ya utoaji wa mkopo wa treka kwa wakulima katika mkoani Ruvuma na mikoa ya jirani kwa lengo la kuwawezesha kuboresha shughuli za kilimo katika ukanda huo. Mkopo huo ambao ni sehemu ya huduma ya NBC Shambani, unatolewa kwa masharti nafuu ambapo mteja atalipa asimilia 25 tu ya mkopo mzima kama malipo ya awali na kiasi kilichobaki atalipa kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi mitano kulingana na makubaliano. Akikabidhi moja ya treka kwa mteja wa kwanza kupata huduma hiyo, Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Ruvuma, Bakari Ally Mketo aliipongeza NBC kwa kuanzisha huduma hiyo ambayo itawawezesha wakulima kupata matrekta kwa urahisi zaidi na kusaidia katika kuongeza uzalishaji mkoani humo.        Mkoa wa Ruvuma ni moja kati ya mikoa inayochangia kwa kiasia kikubwa katika uzalishaji wa mazao ya chakula nchini hivyo huduma hiyo itawawezesha wakulima kuboresha kilimo na kufanya sekta hiyo kuongeza tija zaidi nchini. Kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mkoa huo una jumla ya hekta 4,007,746 za ardhi zinazofaa kwa kilimo ambapo katika kipindi cha miaka mitano 2015/2020 Mkoa umeweza kuzalisha tani 8,547,816 za mazao hadi kufikia mwaka 2020.

Meneja wa Tawi la NBC Songea, Frank Kiranga alisema huduma hiyo ni mahususi kwa wakulima wa aina zote mkoa wa Ruvuma na mikoa jirani na imelenga kuwawezesha kuongeza ufanisi wa shughuli za kilimo mkoani humo. “Ili kupata huduma hii, mteja atatakiwa kuwa na shamba kuanzia hekari moja ambalo lina hati ya kimila au hati ya Kamishna wa Ardhi au mkataba wa mauziano.Pili, mteja atatakiwa kulipa malipo ya awali ya asilimia 25 na kiasi kilichobaki atalipa kwa awamu kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitano,” alisema.

Chacha Marwa Mwikwabe ambaye amekuwa wa kwanza kupata huduma hiyo aliishukuru NBC kwa kuanzisha huduma hiyo ambayo imemuzesha kutimiza ndoto ya kumiliki trekta na kwamba itamuongezea kasi ya uzalishaji katika shughuli zake. Treka moja lina thamani ya Shilingi 62 Milioni na asilimia 25 ni sawa na Shilingi 15.5 milioni kama malipo ya awali.     

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...