Raisa Said,Tanga

Bodi ya Maji Bonde la Mto Pangani katika kuadhimisha wiki ya maji na miaka 31 ya utoaji wa huduma imekabidhi misaada mbalimbali kwa Wazee wanaoishi kwenye Kituo Cha kulelea Wazee Jijini Tanga Kilichopo kata ya Mwanzange .

Baadhi ya Vitu vilivyokabidhiwa na bodi hiyo ni pamoja na Ssabuni,Mchele,Unga , Maharage,Mafuta , Dawa za Meno na Vifaa vya Usafi vyote vikiwa na Thamani ya Sh.500,000.

Akizungumza kwa niaba ya bodi wakati wa wakikabidhi msaada huo , Ofisa kidakio cha mto zigi Mohamed Swalehe alisema Msaada huo ni Sehemu ya Shukrani kwa Jamii ,

" Msaada huu ni Sehemu ya Shukrani zetu kwa Jamii kwakuwa ndio wadau wetu wakubwa , tumeguswa Sana juu ya Wazee wetu Hawa , kwaniaba ya bodi na wafanyakazi wa bonde mto pangani naomba nikabidhi msaada huu" amesema Swalehe

Amesema katika Maadhimisho hayo yaliyoanza Juni 26 na kutamatika Julai 1 wametumia kama fursa ya kutoa elimu kwa jamii juu ya Utunzaji wa Mazingira na vyanzo vya maji pamoja na majukumu ya Bodi ya Maji Bonde Mto Pangani ,

" Kwenye Maadhimisho haya tumepata fursa yakutoa elimu juu ya majukumu ya bonde mto pangani kwenye sekta ya maji pamoja utunzaji wa mazingira na kufahamu utaratibu wa kupata vibali, Sisi ndio Wasimamizi wakuu wa maji na tunawajibika kwenye kila kitu kinachohusu maji hivyo jamii imeweza kufahamu hilo" alisisitiza Swalehe

Kwaupande wake Ofisa Mfawidhi Makazi ya Wazee Wanaoishi kwenye Mazingira magumu , Maria Mwakanyale aliishukuru bodi hiyo kwa msaada huo huku akiomba Wadau wengine kujitokeza kutoa msaada kwa Wazee hao kutokana na mahitaji kuwa mengi,

" Natumia fursa hii kuwashukuru sana bodi ya maji bonde mto pangani kwa msaada huu mliotupatia , tuwaombe nyie mrudi tena lakini pia wadau wengine kujitokeza kutoa Msaada kwa Wazee wetu Hawa , mahitaji ni mengi Sana, hapa tuna Wazee 16 lakini wanaotakiwa ni 40 hivyo wanahitajika wengine lakini pia tunawapatia huduma zote muhimu" alisisitiza Maria



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...