Mratibu wa Mpango mkakati huo ambaye ni Mhadhili wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dk. Feisal Issa, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
SHIRIKISHO la Vyama vya Watu Wenyewe Ulemavu Manispaa ya Ubungo, (Shivyawata) limetoa pongezi kwa Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kwa kutoa mafunzo yaliyopelekea kuandaliwa kwa Mpango Mkakati wa Shirikisho hilo la mwaka 2022/2027.
Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 27, 2022 wakati wa uwasilishwaji wa Mpango huo wa Viongozi wa Shivyawata Manispaa ya Ubungo pamoja na wadau wao kwa lengo la kupitia Mpango na kisha kutoa maoni ya kukamilisha kwa ajili ya utekelezaji.
Mpango huo wa Miaka Mitano umeandaliwa na Wanafunzi Wanaosoma Shahada ya pili ya Uongozi na Usimamizi kwa Kushirikiana na Mkufunzi Dkt. Faisali Issa wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.
Muweka hazina wa Shivyawata Wilaya ya Ubungo, Hemed Omary Ilumbo amesema kutengenezwa kwa Mpango Mkakati huo ni matokeo na mwendelezo wa mafunzo waliyoyapata kutoka Chuoni hapo na ili jamii ione Walemavu ni sehemu yao, kwa pamoja waweze kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chavita Ubungo, Simeon Mwakatobe mbali na pongezi amesema kuwa kiu yao kubwa ni kutaka kujua mpango huo utakavyowasaidia ikiwa ni pamoja kujua ni wapi walipo na wanakwenda.
Awali akifungua mkutano huo Kaimu Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt.Coretha Komba amewataka Shivyawata kujifunza na kutumia Mpango katika kutekeleza majukumu yao vyema huku akiwapongeza Wanafunzi walioshirikiana na Mhadhiri Dkt. Feisali katika kuandaa mpango huo.
Kwa upande Mhadhiri Dkt. Faisal Issa amesema chuo Cha Mzumbe kimekuwa kikiendesha mafunzo mbalimbali Kwa Jamii, Sekta Binafsi, Serikali na Mashirika ya Kijamii.
Amesema mara baada ya kupata Barua kutoka Shivyawata Manispaa ya Ubungo ambao waliomba kupewa mafunzo juu ya utunzaji wa Fedha na Uandishi wa Miradi, kwamba baada ya mafunzo hayo ikabainika kuwa Shivyawata wanahitaji nyenzo ya kufanyia kazi ikiwemo Mpango Mkakati.
"Maombi yao lilipofika kwenye Uongozi wa Chuo ukalifanyia kazi na hatimaye kwa Kushirikiana na Wanafunzi Wanao soma Shahada ya Pili ya Uongozi na Usimamizi wakaanda Mpango Mkakati huo ambao leo tutawakabidhi rasmi" Amesema Dkt. Faisal.
Pamoja na mambo mengine Mpango mkakati huo unamalengo mengi ikiwa ni pamoja na kuongeza uelewa katika jamii.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dk. Coretha Komba, akitoa hotuba yake wakati wa kufungua mafunzo ya namna ya kuendeleza Mpamgo Mkakati wa SHIVYAWATA Wilaya ya Ubungo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...