Na Mwandishi Wetu,Kibaha
LINDA Media Solution kwa kushirikiana na Vyama vya Soka Mkoa wa Pwani wameandaa bonanza la Mpira wa wa Miguu litakalofahamika kama Pwani Sensa Soka Bonanza lililopangwa kufanyika Agosti 14 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Linda Media Solution (LIMSO) Khadija Kalili alisema kuwa tayari wameshapata baraka kutoka kwa Ofisa wa Michezo wa Mkoa Grace Bureta .
"Afisa Michezo alitupongeza kwa kuleta wazo zuri na lenye tija kwa taifa na lengo la kuhamasisha sensa itakayo fanyika Agosti 23 mwaka huu" alisema Kalili.
Aidha aliweka wazi kuwa bonanza hilo litafanyika kwenye viwanja vya Bwawani vilivyopo Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani .
Kalili alitoa wito kwa wadau mbalimbali waweze kujitokeza kuweza kusaidia kwani jambo hili la Sensa ni suala la Kitaifa hivyo hamasa ya kutoa hamasa ni wajibu wa kila mtanzania.
Alisema kuwa kutakuwa na mechi ambazo zitazokutanisha timu mbalimbali ndani ya Wilaya ya Kibaha.
"Pia kutakua na vikundi na wasanii mbalimbali watakaotoa hamasa kwenye viwanja hivyo pia timu itakayoibuka kuwa mshindi wataondoka na zawadi ambazo zitatangazwa hapo baadaye"alisema Kalili.
Afisha Michezo Mkoa wa Pwani Grace Bureta aloyeshika Medali katikati ni Afisa Elimu Mkoa Sara Mlaki na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Mwanasha Tumbo
Afisa Michezo Mkoa wa Pwani Grace Bureta akizungumza na mwandishi wetu wa Mkoani Pwani.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...