Na Said Mwishehe, Michuzi TV

TUME ya Ushindani(FCC) kwa sasa imepiga kambi katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ikiendelea kutoa elimu huku ikiwataka wanaofika kwenye maonesho hayo kufika kwenye banda lao ili kueleza kwa kina kuhusu tume hiyo na majukumu yake.

Akizungumza akiwa katika banda la Tume ya Ushindani ambalo lipo ndani ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mkurugenzi wa Uendeshaji FCC Godfrey Machimu amesema wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu shughuli wanazofanya kwa kutumia Sheria ya Ushindani na Sheria ya Alama.

tuko hapa tangu Juni 28 mwaka huu tukitoa elimu kwa wananchi ili waifahamu FCC na shughuli zake, tunapenda kushukuru kwa muitikio mkubwa ambao umejitokeza kuja kupata elimu , kuielewa FCC na kujua inafanya nini kwa kupitia sheria zake mbili kwa maana ya Sheria ya Ushindani na ile Sheria ya Alama za bidhaa

“Karibuni muweze kuendelea kujifunza FCC tunafanya nini katika upande mzima wa kudhibiti bidhaa bandia, tunafanya nini katika suala zima la ushindani , tunafanya nini katika kuwezesha biashara na uwekezaji,”amesema .

Ameongeza FCC kama taasisi wezeshi wanawasaidia watu wenye mitaji yao wafanyabiashara wakubwa wanaotaka kuwekeza nchini watakuja kama wanamtaji au wanataka kujiunga na makampuni mengine hapa nchini wanaweza kupata kibali cha FFC.

“Pia kama ana biashara yake amesajili nembo yake italindwa na FCC , lakini kama kuna kampuni yake anafikiria ihaifanyi vizuri na angependa kujiunga na kampuni nyingine FCC iko tayari kwa ajili ya kuichunguza na kuangalia kama muunganiko huo hauna madhara katika ushindani

“Kama kuna biashara unafanya katika soko lakini kuna mshindani mwenzako anakufanyia miendeno isiyokubalika kwa mujibu wa sheria FCC iko tayari kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kutoa adhabu iwapo mfanyabiashara atabainika anakinza na sheria ya ushindani.

“Kwa hiyo tuko hapa kwa ajili ya kuwezesha biashara , tuko hapa kwa ajili ya kulinda biashara lakini tuko kwa ajili ya kumlinda mtumiaji.

Kwa upande wake Ofisa Uchunguzi FCC Waambie Malata ameeleza kwenye ushindani , Sheria ya Ushindani namba Nane ya mwaka 2003 inakataza mambo makubwa matatu. Moja ni makubaliano baina ya washindani yanayokiuka ushindani.

“Baadhi ya mambo hayo ni kama makubaliano baina ya washindani kupanga bei, washindani kupunguza uzalishaji au usambazaji wa bidhaa au huduma lakini pia inakataza makubaliano baina ya washindani kupanga njama kwenye zabuni

“Jambo la pili ambalo linakatwaza na Sheria ya Ushindani ni matumizi mabaya ya nguvu ya soko kuwa na nguvu ya soko sokoni kwa wafanyabiashara ni jambo jema na niishara ya kuimarika kwa biashara lakini namna nguvu hiyo inavyotumika inaweza ikasababisha uvunjifu wa sheria ya ushindani.

“Kwa mfano pale ambapo mfanyabiashara mwenye nvuvu sokoni akawa anatumia nguvu hiyo kukataa kutoa huduma au bidhaa kwenye baadhi ya sehemu au kwa baadhi wafanyabiashara , hilo ni kosa kwa mujibu sheria ushindani namba Nane.Lakin mfanyabishara mwenye nguvu sokoni anazuiliwa na sheria ya ushindani kutumia nguvu yake hiyo pale,”amesema.

Aidha ametoa mfano akiwa yeye ndio msambazaji au muuzaji wa malighafi ambayo inatumika kutengeneza bidhaa fulani halafu akawa anawanyima malighafi hiyo kwenda kutengeneza bidhaa hilo ni kosa kwani atakuwa anatumia nguvu yake vibaya , nguvu ya soko vibaya.

Amesema lingine linalokatazwa na Sheria ya Ushindani ni miungano ya kampuni ambazo zinatengeneza au kuimarisha hodhi ya soko, kwa mujibu wa sheria ya ushindani inataka kampuni ambazo zinataka kuungana na thamani yao inafikia bilioni 3.5 zinawajibika kutoa taarifa mbele ya FCC abla hazijaungana ili waweze kufanya uchambuzi wa kisheria na kiuchumi kuona kama muungano huo au kununuana kwao hakutakuwa na madhara ya kisheria au kiuchumi

Wakati huo huo Ofisa wa Kumlinda Mlaji katika Tume ya Ushindani Amina Mjungu ameeleza jukumu mojawapo la tume hiyo ni kumlinda mlaji kuhusu huduma na bidhaa anayoipata sokoni huku akifafanua mlaji ni mtumiaji wa mwisho kabisa wa huduma na bidhaa.

“Katika kumlinda mlaji Tume ya Ushindani inapokea malalamiko ya walaji na kuyapitia na kuyatatua ili kumaliza mgogoro husika.Pia inapokea mikataba ya walaji inayoandaliwa na upande mmoja , mikataba ile inapitiwa katika Tume ya Ushindani na kuhakikisha vile vigezo na masharti vinakidhi viwango kwa pande zote za mlaji na mtoa huduma.

“Hivyo tunawahimiza watoa huduma walete mikataba yao ili tuweze kuisajili katika Tume ya Ushindani kabla ya kutumika sokoni na watumiaji sokoni ambao wamepatiwa huduma ambazo hazipendezi tume inapokea malalamiko yao kupitia ofisi iliyopo Dar es Salaam au Dodoma.Pia wanaweza kuwasiliana nasi kwa namba ya kupiga bure ni 0800110094.”



Mkurugenzi wa Uendeshaji Tume ya Ushindani(FCC )Godfrey Machimu akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kufafanua kwa kina shughuli ambazo zinafanywa na tume hiyo.



Mkurugenzi wa Uendeshaji Tume ya Ushindani(FCC )Godfrey Machimu akiendelea kupanga vipeperushi vinavyoelezea kuhusu shughuli mbalimbali za tume hiyo alipokuwa katika banda lao lililopo kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.





Matukio mbalimbali katika picha ya maofisa wa Tume ya Ushindani wakiwa kwenye banda lao kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.



Ofisa wa Kumlinda Mlaji katika Tume ya Ushindani Amina Mjungu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu majukumu ya tume hiyo.



Maofisa wa Tume ya Ushindani wakiwa makini kufuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkuruguenzi wa Uendeshaji Godfrey Machimu(hayupo pichani).


Ofisa Uchunguzi FCC Waambie Malata akiendelea na majukumu yake kwenye viwanja vya Sabasaba ambapo tume hiyo wameweka banda lao katika ukumbi wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...